Baadhi ya wandishi wa habari kutoka Afrika Kusini wakipiga picha Simba waliotulia chini ya mti katika Pori la Akiba la Selous
Simba wakiwa wamepumzika chini ya mti katika Pori la A Kiba ka Selous
Mwongoza watalii Bw. Mohammed Kabouru akitoka maelezo kwa wandishi wa habari wa Afrika Kusini kuhusu kaburi na historia ya marehemu Selous Mwingereza ambaye jina lake ndilo asili ya pori hilo akiba maarufu hapa nchini na Afrika.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI HAPA
Na: Geofrey Tengeneza - Selous
Kundi la wandshi wa habari tisa kutoka vyombo vya habari vya Serikali na binafsi nchini Afrika Kusini wametembelea Pori la Akiba la Selous na kufurahishwa na vivutio vllivyomo katika pori hilo wakiwemo wanyama kama Simba, tembo, twiga, na ndege wa aina mbali mbali.
Wandishi hao walivutiwa na kufurahia sana kuwaona hasa Simba na tembo kiasi cha miongoni mwao Kulikiri kuwa ni mara yao kwanza kuwaona wanyama hao kwa macho yao wakiwa katika maisha yao ya asili msituni kudaikuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakiwaona katika televisheni na filamu tu.“Nimefurahi sana na mwki umenisisimka sana kuona Simba na tembo kwa mara ya kwanza kwa macho yangu katika historia ya maisha yangu” alisema Bwana Yolisa Mkele, mwandishi wa habari kutoka gazeti la the Times. Aidha walivutiwa sana na ziara ya boti katika mto Rufiji ambapo walifanikiwa kuona idadi kubwa ya kiboko na mamba walioko katika mto huo.
Katika ziara hiyo ya Selous wandishi hao walitembelea na kuona kaburi la Mwingereza Kapteni F.C Selous aliyekuwa akiishi na kufanya shughuli za uwindaji katika eneo hili kabla ya kuuawa na Wajerumani katika vita ya kwanza ya dunia na kuzikwa katika eneo hili lililopewa jina lake kama kumbukumbu na heshima kwake.
Ziara hii ya kundi la wandishi wa habari imeandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania-TTB kwa kushirikiana na Hoteli ya Serena na Shirika la ndege la Fast jet kwa lengo la kitangaza Tanzania nchini Afrika Kusini . Wandishi hawa wako nchini kwa ziara ya siku tatu ya kujionea vivutio vya utalii vya Tanzania hususan vilvyoko katiia pori la akiba la Selous na Zanzibar.
Wakati huo huo wandishi wa habari watano kutoka vituo vya televisheni vya nchi za Ufalme za Kiarabu wanatembelea pia pori la akiba la Selous baada ya ziara yao katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kabla ya kuelekea Zanzibar. Ziara ya wandishi hao imeandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania TTB kwa lengo hilo kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania katika nchi za falme za kiarabu