Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye Msiba wa msiba wa msanii maarufu wa filamu ya vichekesho hapa nchini,Marehemu Saidi Ngamba “Mzee Small” nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam leo Juni 9, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika dua wakati alipokwenda kuhani msiba wa msanii maarufu wa filamu vichekesho Marehemu Saidi Ngamba “Mzee Small” nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam leo Juni 9, 2014.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwafariji wafiwa wakati walipokwenda kuhani msiba wa msanii maarufu wa filamu vichekesho Marehemu Saidi Ngamba “Mzee Small” nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam leo Juni 9, 2014
Mama Salma Kikwete akimpa pole mjane wa Marehemu Saidi Ngamba “Mzee Smal” wakati alipokwenda kuhani msiba wa msanii huyo maarufu wa filamu za vichekesho nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam leo Juni 9, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amejumuika na waombolezaji mbali mbali kwenye Msiba wa msanii maarufu wa filamu za vichekesho nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam leo Juni 9, 2014.Kusoto ni Rais wa Chama cha Filamu nchini,Simon Mwakifwamba na kulia ni Mtoto wa Marehemu Mzee Small,Mahmoud Said Ngamba.
Rais Kikwete akisaini Kitabu cha Maombolezo.
Dua zikiendelea kusomwa kumuombea Marehemu Said Ngamba "Mzee Small".
Rais Kikwete akielezwa jambo na Bw. Mwakifwamba.
MC Mkelle akiongoza shughuli ya Msiba huo.
Waombolezaji Msibani.
Mtoto wa Marehemu Mzee Small,Mahmoud Said Ngamba akionekana ni mwenye Majonzi sana.
Mmoja kati ya watu waliofanya kazi nyingi na Marehemu Mzee Small,Bwana Tupatupa akiongea na vyombo vya habari.
Rais Kikwete akiagana na Mtoto wa Marehemu Mzee Small,Mahmoud Said Ngamba.
Rais Kikwete akiwaaga waombolezaji msibani hapo.
Mama Salma Kikwete akiondika msibani hapo baada ya Kuhani msiba huo.
Waombolezaji msibani.
Jeneza likipakiwa kwenye gari tayari kwa safari ya Mazikoni.
Msafara wa magari na waendesha Bodaboda wakiwa katika barabara ya Segerea Kinyerezi wakati wakielekea Makaburi ya Segerea kwaajili ya Kumpumzisha Kwa Amani Mkongwe wa Sanaa ya Vichekesho Nchini Said Ngamba almaarufu Mzee Small
Gari lililobeba Mwili wa Marehemu Said Ngamba aka Mzee Small (la kwanza) likiwa limesimama kwaajili ya Vijana kuubeba Mwili wake hadi kwenye Makaburi ya Segerea jioni Hii
Vijana wakishusha jeneza lenye mwili wa Marehemu Mzee Small kwaajili ya kuelekea kwenye Makaburi ya Segerea
Vijana wakiwa wamepanga mstari kuanzia Barabara ya Segerea Kinyerezi hadi makaburini kwaajili ya kupokea jeneza lenye Mwili wa Marehemu Mzee Small
Vijana wakiwa wamebeba jeneza lenye Mwili wa Marehemu Mzee Small wakielekea kwenye Makaburi ya Segerea Jioni Hii.
Watu mbalimbali wakisubiri Mwili wa Marehemu kuwasili katika makaburi ya Segerea
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifamba akiwasilika katika eneo la Makaburi ya Segerea jioni hii kwaajili ya kumzika Mzee Small
Mwili wa Marehemu Mzee Small ukitolewa kwenye jeneza tayari kupumzishwa katika Nyumba yake ya Milele katika makaburi ya Segerea.
Watu mbalimbali wakiwasili kwenye makaburi ya Segerea kwaajili ya kumzika Mzee Small. Picha Zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Umati wa watu wakielekea Kupokea Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mzee Small wakati ulipowasili kwenye eneo la Makaburi ya Segerea.
Wanahabari wakitafuta taswira katika mazishi ya Mzee Small katika Makaburi ya Segerea
Picha Zote na Othman Michuzi na Josephat Lukaza.