Msaada wa Matibabu kwa mtoto Maimuna Yahaya Mtoto Maimuna Yahaya (11) anayesoma shule ya Msingi ya watoto wenye mahitaji maalum (wenye ulemavu) ya Irente Rainbow (Lushoto- Tanga) Darasa la pili, anasumbuliwa na tatizo la mifupa na ukubwa wa kichwa tangu kuzaliwa kwake, tatizo lililompelekea kuwa na ulemavu wa viungo na mtindio wa Ubongo.
Mama wa mtoto huyo, Bi. Tunu Juma Maziku amesema amekuwa akimpeleka mwanae huyo Maimuna katika hospitali ya KCMC kwa muda wa miaka 11. Hali ya mtoto inaendelea kuimarika, anaweza kukaa na anaweza kuongea.
Bi. Tunu amekuwa akimpeleka mwanae huyu shule na kumsubiri hadi wamalizapo masomo ya siku na kumrejesha nyumbani kwa muda wa miaka miwili. Bi. Tunu Juma Maziku anasema kwa sasa hali yake ya kiuchumi si nzuri, anashindwa kumpeleka mwanae kuhudhuria matibabu KCMC, hivyo anaomba msaada wa kifedha kwa wasamalia wema ili mtoto wake aendelee na matibabu. Mahali wanapopatikana: Lushoto Mabwawani
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI