Mzee Small enze za uhai wake
Msanii maarufu wa maigizo, Said Ngamba ‘Mzee Small’ anatarajiwa kuzikwa leo saa 10 alasiri katika makaburi ya Tabata jijini Dar es Salaam, baada ya kufariki juzi usiku akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa anatibiwa.
Akizungumza na mtandao huu leo, mtoto wa marehemu, Muhamudu Saidi amesema kuwa kila kitu kinaenda sawa na marehemu atazikwa leo hii.
“Tunamshuru mungu ratiba inaenda vizuri, marehemu atazikwa hukuhuku Tabata katika makaburi ya Tabata, itakuwa saa kumi alasiri” Alisema Muhamudu.