Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

WASIOONA WAOMBA FIMBO NYEUPE

$
0
0
 Mratibu wa Mradi wa Ulingo wa Majadiliano kuhusu ujumuishwaji, Utetezi wa Mahitaji na Haki za Wenye ulemavu wa Macho (Wasioona) Mathias Fwejeje akionyesha Fimbo nyeupe zinazotumiwa na wasiiona, Walemavu hao wa Macho wanahitaji fimbo 110 ili waweze kuepukana na Ajali.
 Mratibu wa ulingo wa majadiliano kuhusu ujumuishwaji wa walemavu wa macho [wasioona] Mathias Fwejeje  katika utetezi wa mahitaji yao na haki katika ngazi mbalimbali za maamuzi.

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUOFYA HAPA CHINI


  Diwani wa kata ya Mnadani Stiven Masangia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Ulingo wa Majadiliano kwa walemavu wa macho waliokutana kujadili namana watakavyofikisha kilio chao kwa serekali ili nao washirikishwe katika utetezi wa haki zao katika maamuzi.
Walemavu hao wa Macho wakiwa ukumbini kwa ajili ya majadiliano hayo.

 Na John Banda, Dodoma
CHAMA cha wasioona Tanzania [TLB] manispaa ya Dodoma kinahitaji msaadawa kununuliwa fimbo nyeupe za kuwatambulisha wanapokua barabarani ilikunusuru maisha ya wanachama wao.Hayo yalisemwa na Mratibu wa mradi wa Ulingo wa majadiliano  kuhusu
uwezeshwaji, ujumuishwaji na utetezi wa mahitaji na haki za wenyeulemavu wa macho Mathias Fyejeje waliokutana miyuji Dodoma.
Fyejeje alisema tatizo hilo la ukosefu wa fimbo nyeupe kwa wasioona nitatizo kutokana na kusababishiwa ajali za mara kwa mara ambapo mpakasasa tayali wanachama wawili wamegongwa japo hawakuathiliwa sana kiasicha kuwafanya kushindwa kutembea.
Alisema kazi kubwa ya fimbo hizo nyeupe ni kumtamburisha asiyeoonaanapokua barabarani kwa madereva na watembea kwa miguu kwani anakuwahawezi kukwepa hatari yoyote bali huyo anayeona anapaswa kufanya hivyokutokana nan a kuiona fimbo hiyo.
Mratibu huyo alisema uhitaji ni fimbo 150 kutokana na idadi yawasioona waliopo katika chama hicho cha Wilaya ambazo kila mojainauzwa kati ya 30,000 na 35,000 kwa moja na hivi sasa wamekwishapokeafimbo 40 toka kwa wahisani mbalimbali na hivyo kusaliwa na 110 mpakahivi sasa.
‘’Umuhimu wa fimbo nyeupe ni mkubwa kwa wasioona kwa sababu pamoja nakumuongoza lakini ni kitamburisho njiani ili waenda kwa miguu namadereva waweze kuwajua kuirahisi hali itakayowaepushia ajali za marakwa mara’’, alisema Fyejeje
Aidha aliongeza kuwa miundo mbinu kwa kwa wasioona ni tatizo hasa kwamajengo na barabara ambapo ameshauri ngazi zote za majengo ziwe navizuizi vya pembeni, Mifeleji  na madaraja yakewe tahadhari ya watuwenye ulemavu huo ili wasipate tabu wanapoitumia.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mnadani manispaa ya Dodoma Stiven Masangia aliyefungua ulingo huo wa majadiliano aliwataka wahisanimbalimbali mbali kuwanunulia fimbo hizo na serikali kuwajengeamiundombinu rafiki ili kuepusha ajali zisizo za lazima kwa wasioona.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles