Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

TUMEDHAMIRIA KUIPASHA TANZANIA KIMATAIFA

$
0
0
 Naibu Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi) mpya wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul Sangawe (Kulia) akila kiapo cha utii na utumishi mbele ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete (Kushoto).
 Naibu Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi) mpya wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul Sangawe akisaini hati ya kiapo.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete (Kushoto) akimkabidhi vitendea kazi Naibu Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi) mpya wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul Sangawe (Kulia) mara baada ya kumuapisha.
Baadhi ya viongozi waandamizi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakisubiri kuapishwa kwa Naibu Katibu Mtendaji mpya wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul Sangawe (hayupo pichani).
Rais Dkt. Jakaya Kikwete (Aliyeinama) akiwapa zawadi watoto wa Naibu Katibu Mtendaji mpya wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul Sangawe (Kulia) mara baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango atakayesimamia masuala ya Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi.
Watumishi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Dkt. Jakaya Kikwete (Watatu kushoto) mara baada ya kumuapisha Naibu Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi) mpya wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul Sangawe (Wapili kulia).
Watumishi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi) mpya wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul Sangawe (Wapili kulia) mara baada ya kuapishwa.
Naibu Katibu Mtendaji mpya wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul Sangawe (Kulia) akizungumza na wanahabari mara baada ya kuapishwa na kukabidhiwa jukumu la kusimamia masuala ya Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi.
Shangwe na vigelegele!
Watumishi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakimpokea kwa shangwe na vigelegele Bw. Paul Sangawe (Kulia) mara baada ya kukabidhiwa jukumu la Naibu Katibu Mtendaji katika Ofisi hiyo ambaye atasimamia masuala ya Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi.Picha zote na Saidi Mkabakuli Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango 

Na Saidi Mkabakuli
Serikali imeweka wazi mkakati wa kuainisha fursa za kipaumbele zitakazoiwezesha kuivusha nchi kikanda na kimataifa kwa kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama inavyobainishwa na Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Miaka Mitano (FYDP I) unaosimamiwa na  Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Mkakati huo umewekwa wazi na Naibu Katibu Mtendaji mpya wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi Bw. Paul Sangawe mara baada ya kula kiapo cha kuitumika nafasi hiyo.
Bw. Sangawe amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuongeza mauzo ya bidhaa na huduma pamoja na kufaidika na misaada kutoka nchi marafiki na mashirika ya kimataifa.
Kwa mujibu wa Mpango Wa Maendeleo Wa Taifa  Mwaka 2012/13 thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma nje ilikuwa dola za Kimarekani 6,796.3 milioni mwaka 2011, ikilinganishwa na dola 5,805.0 milioni mwaka 2010 sawa na ongezeko la asilimia 17.1. hivyo mkakati wetu ni kuongeza hali hii,” alisema Bw. Sangawe.
Kwa mujibu wa Mpango huo thamani ya bidhaa za kukuza mitaji zilizoagizwa toka nje iliongezeka hadi dola za Kimarekani 3,560.5 milioni kutoka dola 2,715.2 milioni mwaka 2010, sawa na ongezeko la asilimia 31.1. Ongezeko hili lilichangiwa zaidi na kuongezeka kwa uagizaji wa mitambo hasa ile ya viwandani.
Aidha, thamani ya uagizaji wa bidhaa za kati iliongezeka hadi dola za Kimarekani 4,139.0 milioni mwaka 2011, kutoka dola 2,741.2 milioni mwaka 2010, sawa na ongezeko la asilimia 51.0. Uagizaji wa mafuta kwa wingi ulitokana na matatizo yaliyojitokeza ya kutozalishwa kwa kiasi kinachohitajika cha umeme unaotokana na maji, hivyo kupelekea mitambo mingi ya mashine kuendeshwa kwa kutumia umeme unaozalishwa na mafuta.
Vilevile, thamani ya mafuta yaliyoagizwa katika mwaka 2011 ilikuwa dola milioni 3,228.7 ikilinganishwa na dola milioni 2,024.2 mwaka 2010. Uagizaji wa bidhaa za matumizi ya kawaida uliongezeka hadi dola 2,128.0 milioni kutoka dola 1,709.2 milioni mwaka 2010, sawa na ongezeko la asilimia 24.5.
Bw. Sangawe ameongeza kuwa Serikali inajikita katika kutambua masoko kwa bidhaa za Tanzania na vyanzo vipya vya uwekezaji katika uchumi wa Dunia na Kikanda ili kuwezesha sekta binafsi kuchangia kufanikisha utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo ili kuwezesha nchi kuchanmkia fursa za masoko ya kimataifa ikiwemo AGOA na nchi za jumuiya za Ulaya.
“Kipaumbele itakuwa ni kutumia rasilimali chache kuchochea uwekezaji wa sekta binafsi pamoja na kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuvutia uwekezaji katika maeneo ya kipaumbele na ya matokeo makubwa,” aliongeza Bw. Sangawe.
Serikali imeaandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ukiwa na lengo la kuwa na mfumo madhubuti wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Lengo la Dira ni  kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles