Katibu wa Michezo kutoka Kampuni ya Proin, Godlisten Anderson akitambulisha viongozi wa kampuni ya Proin Promotions kwa waandishi wa habari wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika leo katika Hoteli ya Southern Sun. Kampuni ya Proin imetangaza kudhamini ligi ya mpira wa miguu kwa Wanawake inayotarajiwa kuanza Mwezi wa Nane.
Rais TFF, Mh Jamal Malinzi na Mwenyekiti wa makampuni ya Proin, Mh Johnson Lukaza wakitia saini katika mkataba wa makubaliano ya udhamini wa ligi ya mpira wa miguu kwa wanawake itakayoanza mwezi wa Nane.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Raisi wa TFF, Mh Jamal Malinzi (kushoto) akibadilishana mkataba wa udhamini na Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Mh Johnson Lukaza (katikati) mara baada ya kumaliza kutiliana saini katika mikataba hiyo mbele ya waandishi wa habari leo katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Southern Sun.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Cha Wanawake, Bi Lina Muhando akiongea na Waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Sourthen Sun wakati Kampuni ya Proin ilitangaza kudhamini ligi ya wanawake inayotarajiwa kuanza Mwezi wa Nane
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Mh Johnson Lukaza akijibu maswali ya waandishi wa habari leo katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hotel ya Southern Sun.
Rais wa TFF, Mh Jamal Malinzi akiteta jambo na Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Mh Johnson Lukaza wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar Es Salaam.
Mwandishi wa Habari kutoka gazeti la Jambo leo, Bi Asha Kigundula akiulizwa swali katika mkutano huo.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Na Josephat Lukaza - Dar Es Salaam
Kampuni ya Proin Promotions leo imetangaza rasmi kudhamini ligi ya mpira wa miguu kwa wanawake inayotarajiwa kuchezwa mnamo mwezi wa nane mwaka huu Jijini Dar Es Salaam ambapo itahusisha timu za wanawake washindi kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Proin Promotions imeingia mkataba wa miaka miwili kwaajili ya kudhamini ligi hiyo. Proin Promotions inaendelea na lengo lake la kusaka vipaji katika Mpira wa miguu kwa wanawake ambapo sasa Proin imeanza kusaka vipaji katika Tasnia ya Filamu nchini kwa kuanzisha shindano liitwalo Tanzania Movie Talents.
Akiongea na Waandishi wa Habari leo Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Mh Johnson Lukaza amesema Kuwa Sasa imefika wakati Kuanza kuibua vipaji vya mpira wa miguu kwa wanawake ambapo ndio lengo kubwa la Kampuni yake hiyo ya Proin Promotions. Vilevile aliongezea Kampuni yake tayari imeshaanza mchakato wa kuibua vipaji vya Kuigiza kwa Kuanzisha Shindano lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents ambapo kuanzia tarehe 17 Mwezi huu kipindi cha kwanza kitaanza kurushwa hewani katika kituo cha Runinga cha ITV kuanzia Mida ya Saa Nne Usiku na sasa ni zamu ya Watoto wa kike kung'ara katika Mpira wa Miguu.
Vilevile Kampuni ya Proin Promotions Imesema inawakaribisha makampuni mengine pia kujitokeza kudhamini ligi hii ya mpira wa miguu kwa wanawake ambapo itasaidia kuibu vipaji na kuifanya timu ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars kupata wachezaji wenye viwango vya juu ambao wataliletea Taifa la Tanzania sifa na wao pia kuweza kuuzika kimataifa.