Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Ghalib Bilal akiwa na moja ya tuzo zilizotolewa kwa walimu wa Shule zilizofanya vizuri katika Elimu 2013 wakati wa kilele cha wiki ya Elimu, Kushoto ni Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Dkt Shukuru Kawambwa na Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi.
Makamu wa Rais Dkt Ghalib Bilal akimpatia cheti Mwanafunzi Nelson Athon wa shule ya sekondari ya Kizilego iliyopo mkoani Bukoba baada ya kufanya vizuri mwaka jana.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Msalato ya Dodoma akiwa ameshika mfano wa hundi ya Milion 3 zilizotolewa na Selikari kama motisha kwa shule hiyo kupandisha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi kwa mwaka 2012/ 13 motisha hiyo imetolewa kwa jumla ya shule 14 za sekondari na 46 za msingi nchini, wakati kilele cha maadhimisho ya wiki ya Elimu.
Mshaili wa sanaa ya Rugha katika Muziki Mrisho Mpoto na Banana Zoro wakitoa Burudani katika kilele cha wiki ya Elimu iliyofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma.
Wanafunzi shule za msingi na Sekondari wakiwa majukwaani na mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Elimu yaliyofanyika Dodoma.
Wanafunzi wa shule mbambali za msingi na Sekondari wakiwa wamezagaakutembelea mabanda ya maonyesho ya wadau wa Elimu katika siku ya mwisho ya maadhimisho ya wiki ya Elimu kabla ya kufungwa.
Wanafunzi na walimu ambao shule zao zimefanya vizuri wakiwa katika jukwaa maarumu walipokuwa wakisubili tuzo na zawadi mbalimbali zilizotolewa na Makamu wa Rais Dkt Ghalib Bilal wakati wa kilele chawiki ya Elimu iliyohitimishwa jumamos Mei 10, 2014 iliyofanyika kitaifa Dodoma.