Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

YAJUE MAMBO SABA(7) WANAYOFANYA WATU WALIOFANIKIWA KITAALUMA

$
0
0


Taaluma na mfumo wetu unaweza kuwa tofauti kidogo ila mambo huwa yanakwenda kwa mlinganyo fulani ambao unatakiwa kuufahamu, hasa kwenye taasisi binafsi ambazo kinachoangaliwa ni utendaji na uwajibikaji madhubuti. Kwenye kila taaluma unaweza ukaamua kuwa abiria wa kawaida ambaye unatizama dereva anafanya nini na unakuwa unafurahia kwa sababu wewe huhusiki katika nyadhifa za juu. Ila kwa dereva (mmiliki, wakurungenzi) yeye huhakikisha anaongoza kila kitu kinakwenda kama kinavyotakiwa. Kama unataka kuwa dereva au abiria jukumu ni la kwako, unachukua maamuzi gani? Unapotaka kufanikiwa kitaaluma hebu fuatilia watu waliofanikiwa kitaaluma wanafanya nini;

1. Unatakiwa ujue kwamba wewe ni bidhaa au biashara ya mtu
Taaluma yako ina mtaji ndani yake, hivyo unatakiwa kujua una amini kama mtaji katika taaluma yako, nani anaweza kukulipa zaidi ya mwingine? kama hauna taaluma inayohitajika ni bora uanze kutafuta ya kwako ambayo ambayo watu watakulipa kwa ajili ya hiyo taaluma.

2. Unatakiwa kujua namna ya kutumia fursa vizuri
Unatakiwa ujue namna ya kukubaliana has a kwenye mshahara wake. Mwajiri anatafuta mtu atakaye mtumia kwa bei nzuri, na wewe uwe makini sio kubebwa tu kwa hela yoyote. Kumbuka hufanyi kazi kwaajili ya mwajiri ila unafanya kazi pamoja na mwajiri.

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

3. Fanya kazi zako vizuri
Kumbuka kufanya kazi vizuri ni bora kuliko kufanya kitu kipya. Zingatia kujenga na kuboresha ujuzi na ufanisi wake. Unatakiwa uwe unajua baadhi ya vitu vizuri sana.

4. Fanya kazi na watu ambao wamekuzidi uwezo
Tafuta watu waliokuzidi uwezo na ufanye kazi nao. Tafuta makampuni ambayo yanafanya kazi kwa viwango via juu, ujue namna ambavyo hutoa huduma zao, au bidhaa za na ukiweza tanya nao uhusianao kibiashara ili uweze kukua namna ya utendaji katika kazi au huduma.

5. Fuatilia malengo na dira ya Kampuni
Kama unataka uwe mtu uliyefanikiwa kitaaluma hutakiwi kwenda kichwa kichwa au bila kujua dira na malengo ya kampuni hiyo. Unatakiwa ujue kampuni hiyo inatekeleza malengo yapi na ni nini dira yao ili uweze kufanya kazi na kutoa huduma kulingana na mule wanakokwenda. Ukiweza kufanya vizuri zaidi ya pale wanapofikia uwezekano wa kukuweka katika viwango vizuri zaidi ni rahisi. Wanahitaji mtu ambaye anajua wapi wanakwenda na mtu ambaye anaweza kutoa huduma kulingana na vigezo vyao.

6. Uwe kwenye nafasi ambapo mambo yasipokwenda vizuri uondoke
Jitahidi upate mshahara au fedha ya kukutosha kukaa mwaka mzima bila kazi, kwa kuwa kila kazi ni ya muda tu unaweza ukaipoteza wakati wowote. Hivyo ukitaka kuacha kazi hakikisha kifedha unaweza kukuaa muds mrefu bila kuingiza kipato na mambo yakaenda.

7. Unahitaji uzoefu wa kukuwezesha kwenda mbele zaidi
Hakuna kushindwa ambako mtu hushindwa kabisa, tunapata uzoefu, tunajifunza na kukua kitaaluma. Achana na kufanya kazi sehemu ambazo unajua hautafukuzwa au hautaacha kazi hive karibuni hizo ni dalili za kwamba utapata wakati mgumu wa kusonga mbele kitaaluma kama unataka kufanya maamuzi magumu. Unahitaji kujifunza vitu vipya, kukosea ndio kunakufanya uweze kujifunza na kuendelea mbele.

Je unamiliki taaluma yako? au watu wengine ndio wanamiliki taaluma yako? Amua leo kumiliki taaluma yako mwenyewe kwa kufanya maamuzi sahihi na kusonga mbele. Uwe tayari kuacha kazi na hiyo ofisi uende ukafanye kitu bora zaidi kuliko hicho.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>