Malori na Mabasi yakiwa kwenye msururu mrefu mara baada ya kushindwa kuendelea na safari kwa takribani masaa zaidi ya nane katika eneo la Manzese lililopo Kilwa barabara ya Dar Es salaam kuelekea Mtwara hapo jana kutokana na eneo hilo kuharibiwa vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha na kupelekea magari zaidi ya mia kukwama
Baadhi ya wasafiri kwenye mabasi yaendayo Dar Es Salaam kutoka Mtwara, Lindi na Kilwa na yale yatokayo Jijini Dar Es Salaam kuekelea mikoa ya Kusini wakiwa wamesimama kushuhudia juhudi zinazofanya na vijana wa eneo la Manzese na baadhi ya madereva wa malori na mabasi pamoja na abiria kuhakikisha wanasaidia magari kuvuka ili kuweza kuendelea na safari zao.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wasafiri na wakazi wa Eneo la Manzese wakishuhudia greda lililofika kwaajili ya kusaidia kusawazisha eneo hilo na kutoa magari yaliyonasa kutokana na eneo hilo kujaa maji na tope zito yaliyosababisha magari kukwama kwa takribani masaa zaidi ya nane hapo jana.
Mabasi yatokeayo Mikoa ya Kusini kuelekea Bara yakiwa yamekwama katika eneo la Manzese - Kilwa kutokana na barabara kuwa mbovu katika eneo hilo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kupelekea kusababisha magari zaidi ya mia kunasa na kutoendelea na safari zao kwa zaidi ya masaa nane.
Greda likiondoa tope na kusawazisha eneo hilo ambalo lilileta usumbufu mkubwa sana kwa watumiaji wa barabara ya Dar Mtwara na kupelekea magari zaidi ya mia kukwama katika eneo hilo lililoaharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Malori yakiwa kwenye msururu.
Greda likilivuta basi lililokuwa likitoka Mtwara kuelekea Dar Es salaam mara baada ya kunasa katika tope zito
Vijana wakirekebisha barabara kwaajili ya kuinasua gari aina ya Toyota Harrier iliyonasa katika Eneo la Manzese kutokana na barabara kuharibiwa vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha.BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI»