Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

KWANINI BAADA YA CHUO UNATAKIWA KUENDELEA KUJIFUNZA?

$
0
0

Umemaliza masomo, vitabu unaendelea kuvifunga na unataka kuanza maisha mapya na utu uzima unaingia. Lakini mambo yanaenda, unapoendelea kujifunza ndipo furaha na kufanikiwa katika taaluma kunaanza. Hebu fikiri unapoondokana na mitihani na kusoma darasani unajifunza vitu vingi na mambo mengi. Unajifunza vitu ambavyo ni kidogo mwishowe unakuwa na weledi wa kitu fulani. Unapoendelea kujifunza unaongeza ufahamu zaidi, si kwaajili ya fedha tu bali ni kwa ajili yako na kufanikiwa katika maisha.
Maisha ndio kwanza yameanza, labda umeingia mjini kwa mara nyingine uko mtaani. Unahitaji kujifunza desturi na tamaduni katika eneo ambalo unaanza maisha. Maisha yanaenda tofauti na jinsi ambavyo ulikuwa unaishi chuo hivyo unatakiwa kuwa makini. Kutana na watu tofauti na ujifunze kutoka kwao, ila chambua kila kitu ambacho kitakufaa kwa maisha yako binafsi.
Faida ya kuendelea kujifunza ni kujua mazingira na vitu tofauti na vile ambayo ulikuwa navyo chuoni. Mazingira ya chuo ni tofauti na mtaani, mtaani hakuna migomo kisa chakula kimepanda bei au vinginevyo ila unahitaji kupambana na mazingira halisi.

 ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Unachotakiwa kujifunza ni kwamba unahitaji kujihudumia kwa kila kitu endapo utapata kazi au hautapata kazi. Kwahiyo wakati upo chuoni unahitaji kuanza kufikiri , je ninaenda kuishi vipi bila ya mkopo wa serikali? je unapambana vipi na mazingira utakayo yakuta? Je ninahitaji nini ili niweze kuishi na watu nitakaowakuta?
Je kuna kitu ambacho nimejifunza chuoni ninaweza kukiweka kwenye matendo na kikafaa? au wewe ulikuwa mtu wa kuigilizia tafiti mlizokuwa mnaambiwa mfanye? Jifunze kwamba huku mtaani ni zaidi ya cheti kinachohitajika, kunahitajika watu wenye uwezo wa kufanya kile ambacho wamejifunza hivyo cheti chako kitajaribiwa na ukishindwa hakuna atakayekuthamini tena.
Itabidi ujifunze kuishi na watu wengine tofauti na wanafunzi, kuwa mwanafunzi kuna mambo mengine hufanyika tofauti na hali halisi ya huku mtaani. Unahitaji akili ya kutambua kuwa unaenda kwenye mazingira tofauti hakuna mkumbo tena. Andaa akili na mazingira ya kuwa siku moja utakuwa na familia, je wewe ni mtu ambaye unaweza kuishi na familia yako binafsi? Kwa ufupi je unaweza kuongoza familia yako mwenyewe? Je umefikiria kuhusu mwenzi wako na awe wa namna gani?
Tafuta Uzoefu wa kile unachosomea, wakati ukiwa chuo tafuta sehemu ambayo unaweza kuweka kwenye matendo kile ambacho unasomea ili uwe na ujuzi wa hicho kitu. Hapa nazungumzia nje ya kwenda kwenye mafunzo kwa vitendo fanya kitu zaidi ya hapo, huwezi kujua kitakusaidiaje utakapoingia mtaani. Kitu cha msingi ni kuendelea kujifunza zaidi ya mambo ya darasani ndipo uelewa wako utakuwa mkubwa kuliko wenzako katika taaluma hiyo hiyo.

na Bongo 5


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>