Mshambuaji wa timu ya Liverpool na Uruguay Luis Suares amechaguliwa tena na chama cha waandishi wa habari wa michezo Uingereza kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya England.
Wiki mbili zilizopita Luis Suarez alitangazwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya England kupitia chama cha wanasoka wanaocheza EPL.
Kupitia twitter ya Liverpool wamesema:Congratulations @luis16suarez, who has been voted 2014 Footballer of the Year by the Football Writers’ Association. Suarez, 27, aliwashinda kwa kura nyingi wachezaji wengine akiwemo nahodha wa Liverpool na England Steven Gerrard.
Mabao 30 aliyofunga msimu huu kwenye EPL yameiweka Liverpool kwenye nafasi ya kutwaa ubingwa wa Barclays Premier League baada ya miaka 24.