Baadhi ya askari Polisi wakiutoa mwili wa askari Polisi kwenye Wodi namba moja aliyeuawa kwa kupigwa risasi na majambazi huko katika Tarafa ya Ussoke wilayani Urambo askari huyo aliyefahamika kwa namba F.5179 PC Jumanne, walipigwa risasi wakiwa na askari mwenzake ambaye pia alifariki papo hapo namba G.3388 PC Shaban.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan Kaganda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la mauaji ya askari Polisi wawili ambao waliuawa wakati wakijitayarisha kukabiliana na Majambazi watatu waliovamia nyumbani kwa mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina la Ibrahimu Mohamed mkazi wa Ussoke ambapo walipora zaidi ya shilingi milioni moja na laki mbili pamoja na vocha za simu zenye thamani ya shilingi laki moja na ishirini elfu.Kamanda Suzan alisema majambazi hayo yalikuwa yakitumia bunduki aina ya SMG.