Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

BASI LA SUMRY LAUA KWA KUGONGA WATU 13 AKIWEMO ASKARI WA USALAMA BARABARANI MKOANI SINGIDA

$
0
0
http://3.bp.blogspot.com/-IznzeO4vDN0/UCUn5TRoxJI/AAAAAAAACis/f4SuEtsRyJo/s1600/AJALI+YA+BASI+LA+SUMRY+DAR-MNZ+BARABARA+KUU+DODOMA-MOROGORO+PIX+NO+5.JPGWATU 13 akiwemo askari wa kikosi cha usalama barabarani wamepoteza maisha baada ya kugongwa na basi la kampuni ya Sumry lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar katika kijiji cha Ikungi mkoani Singida. 

Ajali hiyo ilitokea baada ya ajali ya kwanza iliyolihusisha lori lililomgonga mwendesha baiskeli aliyepoteza maisha papo hapo na wakati wananchi wakiwa wamekusanyika eneo hilo la ajali huku trafiki akiendelea kupima ajali hiyo, lilitokea basi la kampuni ya Sumry na kuwagonga watu hao pamoja na trafiki na kupelekea jumla ya watu 14 kupoteza maisha eneo hilo. 

Basi hilo lililokuwa likitokea Kigoma kwenda Dar halikuweza kusimama eneo hilo mpaka dereva wake alipokwenda kujisalimisha kituo cha polisi Ikungi, Singida. 

Miili 14 ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Singida pamoja na majeruhi wawili waliopelekwa hospitalini hapo.

MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>