Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

ASKARI TRAFIKI SITA WATIMULIWA WA MKOANI MBEYA

$
0
0


Kamanda wa Polisi  Mkoani 
Mbeya  SACP Ahmed Msangi

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limewafukuza kazi Askari sita  wa kikosi cha Usalama barabarani  Wilaya za Rungwe na Mbeya kwa tuhuma za kuomba,kushawishi na kupokea rushwa.
Kamanda wa Polisi  Mkoani Mbeya  SACP Ahmed Msangi amewatataja Askari hao kuwa ni pamoja na waliokuwa wakifanya kazi wilaya ya Mbeya barabara ya Mbeya/Tunduma eneo la Songwe ni Koplo  Jonson, PC Rymond na PC Simon.
Msangi amewataja wengine kuwa ni pamoja Sajini Hezron,PC Shaban na PC Kajolo ambao walikuwa wanafanya kazi barabara ya Mbeya/Rungwe wilaya ya Rungwe.
Askari hao walikuwa wanakabiliwa na makosa hayo na walifikishwa katika Mahakama ya Kijeshi na Hukumu kutolewa Aprili 24 mwaka huu na kupewa adhabu ya kufukuzwa kazi.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Aidha Kamanda Msangi amesema Jeshi lake halitasita kuwafukuza kazi Askari watakaokwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi na Askari yeyote atakayekwenda kinyume atakumbwa na adhabu kali ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi au kufikishwa mahakamani.
Askari wengine waliofukuzwa kazi hivi karibuni ni pamoja na PC James Kagomba ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa kutumia silaha,WP Prisca Kilwai anayekabiliwa na kesi ya wizi wa mtoto.
Wengine wliohukumiwa kifungo cha mwaka mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia ni DC Marcelino Venance mwenye namba 8084,PC Juma Idd mwenye namba 3117 na Askari wa Mgambo MG Jackson Mwakalobo ambao walidaiwa kusababisha kifo cha mwanafunzi Dentho Kajigili aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari Ivumwe ya Jijini Mbeya. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>