Uchafu huu umetupwa na mtu ambaye hakufahamika kirahisi kwenye barabara inayotokea daladala za kituo cha Mwenge jijini Dar es Salaam. Cha kusikitisha uchafu huu umetupwa karibu sana na kituo cha polisi cha Mwenge na kuwa kero kwa wafanyabiashara wa eneo hili.
Hii ndio hali halisi ya uchafu uliotupwa katikati ya barabara inayoelekea kwenye Stendi hiyo ya Mwenge. Wahusika mnaliona hili?