Mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete akiwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dodoma walipokuwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya vipimo na tiba kwa ajili ya ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya Uzazi kwa wanawake iliyofanyika Wilayani Bahi.
Mke wa Rais Jakaya Kikwete Mama Salma Kikwete akisalimaiana na Afsa wa idara ya Afya ya Jamii wa Shirika la DCMC Katrin Boehl ambao wanashirikiana moja kwa moja kwenye uendeshaji wa mradi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa wanawake, alipofika kuzindua Mradi huo.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mama Salma Kikwete akisalimiana kwa kugongeana mikono na Wananchi wa Wilaya ya Bahi alipohudhuria uzinduzi wa kampeni ya vipimo na tiba kwa ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya kizazi.
Dakitari Bingwa wa Macho wa Ona Network INC inayotoa huduma za Afya ya Macho Vijijini akimueleza jambo Mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete aliyefika Wilayani Bahi Kuzindua Kampeni ya Vipimo na Matibabu kwa ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya Kizazi.
Wanawake wanaosumbuliwa na macho wakiwa katika viwanja vya shule ya msingi Bahi walipofika kupata vipimo vya macho na magonjwa menginevilivyokuwa vikitolewa bure wakati wa uzinduzi wa kampeni ya tiba ya ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya kizazi inayotolewa bure.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bahi wakiwa na Mabango yenye ujumbe Tofauti wakati wa uzinduzi wa Vipimo Vya Saratani ya Shingo ya Kizaziiliyofanyika juzi katika Viwanja vya Shule ya msingi Wilayani humo.