Prof. Anna Tibaijuka akiongea na mke wa Rais Salma Kikwete mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Chimwaga kwenye kongamano la wanafunzi wa wakike wa vyuo vikikuu.
Mke wa Rais wa Tanzania Salma Kikwete akipanda mti nje ya jengo la utawala la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) alipoenda kuzindua kongamano la wanafunzi wa kike lililofanyika juzi.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Salma Kikwete akilisakata Rhumba pamoja na wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu waliokutana kwa ajili ya kongamano lililofanyika katika ukumbi wa chimwaga uliopo katika Chuo Kikuku cha Dodoma (UDOM).
Baazi ya wanafunzi wa chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakimsubili Mke wa Rais Salma Kikwete aliyekuwa amefika chuoni hapo kuhudhuria Kongamano la wanavyuo wanawake lililofanyika mwishoni mwa wiki hii.
Na John Banda, Dodoma
WASICHANA wasomi wa vyuo vikuu wametakiwa kujiepusha na uhuni wa kingono na badala yake wazingatie malengo yaliyowapeleka masomoni ili kuepuka kuzitia hasara familia zao na taifa kwa ujumla
Haya yalisemwa na Mke wa Rais Jakaya Kikwete, Salma Kikwete alipokuwa azindua Kongamano la wanafunzi wasichana wa Vyuo vikuu lilofanyika Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) juzi
Mama Salma alisema kumekuwa na tabia ya wasichana wa vyuo vya elimu ya juu kuwa na wanaume watatu kwa wakati mmoja ambao wao huwaita moja wa pamba yaani mavazi, mwengine ni wa kumsaidia darasani kimasomo na mwingine wa ukweli yaani anayempenda huku wakijidanganya kuwachuna na
kumbe wanachunwa wao kutokana na kila mtu kuwa na nguvu yake wakati wa tendo
Salma alisema wasichana hao wanatakiwa kujua wapo masomoni kwa malengo maarumu ya kuzisaidia familia, jamii zinazowazunguka na taifa kwa ujumla mara baada ya kumaliza masomo yao hivyo wanatakiwa kujiepusha na starehe zisizo maana zinazotokana na kujirahsisha.
Mke huyo wa Rais mwenye fani ya ualimu aliwataka wasichana hao kuhakikisha wanajitambua kama ni wanawake wenye maumbile tofauti na wanaume na hivyo kuhakikisha wanaiweka miili yao kuwa katika uthamini mara baada ya kuvunja ungo kinyume cha hapo ni mimba na magonjwa ya ngono.
Aliwafananisha wasichana na madini aina ya Lulu yanayopatikana ndani ya samaki chaza anaishi miambani kwenye kina kilefu cha bahari na hivyo kutokana na ugumu wa upatikananaji wake mara nyingi ilikuwa ikitumiwa na wake wa wafalme pekee.
''Wasichana zitunzeni Lulu zenu kwaajili ya manufaa yenu ya baadae acheni tabia za kujihusisha na ngono, ni lazima mjua kwamba familia zimejifunga mkanda kukusomesheni ili mje kuzisaidia hivyo wanaume
mliokutana nao vyuoni mjue kabisa sio hao watakao kuwa wenzi wenu katika maisha wanawapotezea muda wa masomo bure'', alisema
Aidha Mama Kikwete Aliwaambia wasomi hao wa kike wa vyuo vikuu kuwa wanatakiwa kuwa na tabia njema ambayo itawafanya wapate mafanikio katika kila Nyanja watakazopitia na hatimae kuwa viongozi wazuri wa familia na taifa hili.
Salma alizindua Kongamano hilo lililoandaliwa na Wanafunzi wa chuo Kikuu cha Dodoma lilivikutanisha vyuo vikuu vya Serikali za Mitaa, Madini, Mtakatifu Yohana, CBE na Mzumbe walikuwepo Dodoma kutembelea
Bunge la bajeti na wiki ijayo anatarajia kuzindua mpango wa upimaji na matibabu ya salatani ya shingo ya uzazi kwa wanawake Wilayani Bahi juzi.