Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mmoja wa baadhi ya abiria waliokwama baada ya barabara ya Chalinze-Dar es Salaam kuharibiwa vibaya na mafuriko
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Mkewe Mama Salma Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza wakikagua athari za mafuriko zilizoharibu vibaya barabara ya Chalinze- Dar es Salaam eneo la Ruvu Darajani leo.Mamia ya abiria walikuwa wamekwama kutokana na mafuriko hayo.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Rais akisalimiana na kuzungumza na wanafunzi na mtoto aliyemfuata na kumsalimia.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete wakikagua athari za mafuriko maeneo ya Ruvu Darajani na Visiga
Picha na Freddy Maro