MAHAKAMA Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imesema itatoa uamuzi wa kuliondoa shitaka la kukaidi amri halali iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam au la dhidi ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda Desemba 11, mwaka huu.
Umuzi huo ulitolewa leo na Jaji Rose Teemba baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kuhusu maombi ya marejeo ya kupinga kuondolewa shitaka hilo yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Sheikh Ponda.
Kabla ya uamuzi huo kutolewa upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Benard ess Zakaria, walidai kuwa wanapinga maombi hayo kusikilizwa kwa sababu kiapo kilichoambatana nayo kinamapungufu ya kisheria.
Kongola alidai kuwa kiapo kinabeba hoja za maneno ya maombi hayo na kwamba kama kimekosewa yatakuwa batili hayafai kusikilizwa na mahakama yatupwe.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
“Katika hati ya kiapo hicho hakuna baadhi ya vipengele ikiwemo tarehe ya kuwasilisha kiapo na muapaji aliapa kwa mtu anayemfahamu au alitambulishwa na nani… kosa hilo haliwezi kurekebishika kwa hiyo maombi yaliyopo mbele yako Mtukufu Jaji ni batili” alidai Kongola wakati akitoa hoja za kupinga maombi ya Ponda yasisikilizwe.
Akifafanua zaidi wakili huyo alidai kuwa Jamhuri inapinga maombi hayo kusikilizwa kwa sababu yamekiuka kifungu namba 8 cha sheria inayosimamia viapo.
Akijibu hoja za Jamhuri, wakili wa utetezi Juma Nassoro alidai kuwa pingamizi la Jamhuri halina misingi ya kisheria na kwamba kiapo kinaonyesha maombi yaliwasilishwa Oktoba 10, mwaka 2013.
Juma alidai kuwa aliyekula kiapo hicho ni Obadia G. Hamidu na mtoa kiapo aliyetajwa kwa jina moja, Kifunda ni wakili anayemfahamu muapaji vizuri na kwamba hoja za utetezi ni sahihi kwa mujibu wa kifungu namba 8 cha sheria inayosimamia viapo.
Baada ya mabishano hayo ya kisheria Jaji Teemba alisema uamuzi wake utatolewa Desemba 11, mwaka huu.
CHANZO: MICHUZI BLOG
CHANZO: MICHUZI BLOG