Barabara ya Mwai Kibaki leo asubuh ilikuwa na foleni kubwa kutokana na maji kujaa barabarani na kupelekea magari kukwama katika barabara hiyo hii imesababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha
Magari yakipita taratibu katika eneo hilo
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Hapa ni makutano ya Barabara ya Morogoro na Lumumba ambapo ujenzi wa Barabara umekamilika lakini tatizo la kujaa kwa maji linaendelea.
Upepo mkali uliangusha baadhi ya Miti.
Hali ya maji katika bonde la msimbazi, serikali imeiifunga barabara ya Morogoro kutoka magomeni hadi Faya, kutokana na maji kuvuka kima cha Daraja la Jangwani.
Hii ndio hali halisi ya barabara nyingi za Jijini Dar es Salaam kwenye kipindi hiki cha mvua