Baadhi ya Wakazi wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Mwenyekiti wa Bongo Movie(Steve Nyerere) na Single Mtambalike wakiwa pembeni ya Mkurugenzi wa Msama Promotions Limited Bw Alex Msama kwaajili ya kumpa pole na kumfariji mara baada ya kupata ajali wakati akitokea Dar Es Salaam kuja Dodoma, ajali iliyotokea Ipagala Mwisho Kilometa chache tu kufika Dodoma Mjini.Picha na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog.
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Bw Alex Msama amepata ajali mbaya eneo la ipagala Mwisho muda mfupi uliopita na Katika ajali hiyo iliyohusisha Mwendesha Bodaboda na gari ya Mr Alex Msama.
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Bw Alex Msama amepata ajali mbaya eneo la ipagala Mwisho muda mfupi uliopita na Katika ajali hiyo iliyohusisha Mwendesha Bodaboda na gari ya Mr Alex Msama.
Baada ya ajali hiyo kutokea Waliweza kukimbizwa Katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma Kwa matibabu zaidi na wameweza kupatiwa matibabu na kupelekwa katika Chumba cha X-ray na mpaka naondoka Hospitali hapo majibu ya x-ray bado hayajatoka lakini hali zao sio mbaya sana.
Katika ajali hiyo iliyohusisha gari na bodaboda hakuna aliyepoteza maisha. Bw Msama amepata majeraha madogo madogo sehemu za mikononi lakini pia na kusikia maumivu katika kifua. Huku mwendesha bodaboda nae hali yake sio mbaya sana japokuwa ana maumivu katika sehemu mbalimbali za mwili na wagonjwa wote wanaendelea na kupewa matibabu katika hospitali ya Mkoa Dodoma.
Taarifa zaidi zitakujia hivi punde
CHANZO: LUKAZA BLOG
Taarifa zaidi zitakujia hivi punde
CHANZO: LUKAZA BLOG