Msanii mkongwe wa Hip Hop, Godfrey Tumaini aka Dudu Baya, amekanusha kuhusika katika tukio la kumkata mama yake mkumbwa sikio kama ilivyoripotiwa na mdogo wake wiki hii
Akizungumza na ‘You Heard’ ya Clouds FM jana mdogo wake wa tumbo moja na Dudu Baya, Mueta amesema juzi majira ya saa nne asubuhi jijini Mwanza rapper huyo alienda kwa mama yake mkubwa na kumkata sikio.
“Dudu kafanya hivyo, nimejaribu kufuatilia ,duh inasikitisha,lakini sasa ndio hivyo kashafanya, kaenda kwa mama mkubwa kule ,kaenda kamkata sikio jana (juzi). Sababu haijulikani, sababu gani kaenda kufanya kitu kama hicho. Hata kama alikuwa na sababu sidhani kama ni busara kwenda kumkata,kwa madai kuwa mama mkubwa alikuwa anamloga Dudu mambo ambayo hayana hata msingi kwa ujulma,kwasababu hata ukiangalia anamloga kivipi!! Yeye ni mtoto haumwi na hana matatizo yoyote. Mwanae sio mgonjwa ni mzima tu, mimi nikashindwa kuelewa, sasa bibi mkubwa akawa ameleta mtafaruku kwasababu wanae hili suala hawajakubaliana nalo,ikanibidi mimi niende nikazungumza nao pale,tukaenda polisi tukaongea na maaskari, basi tukajua namna ya kumtafuta. Kwahiyo akikamatwa ndio ataeleza alifanya hilo tukio kwa sababu gani, au labda pengine aliagizwa na nani,” alisema.kwa na kudai kuwa yeye ni mtu anayeitambua dini yake.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Dudu Baya ameuambia mtandao huu baada ya kuzagaa kwa taarifa ya kutafutwa na polisi wa Mwanza kutokana na tuhuma za kumkata mama yake mkubwa sikio: Unajua hata mimi nashangazwa na hizi taarifa za kutatanisha,mimi Godfrey Tumaini nimesomea dini sana,natambua kipi kibaya na kizuri,siwezi fanya tendo kama hilo kwa mama yangu mkubwa hata siku moja. Unajua sisi ukoo wetu tuna matatizo sana inawezekana kafanya mtu mwingine ila sio mimi.Mimi hapa juzi kati nilipigiwa simu na ndugu zangu pamoja na mama yangu wakaniambia mama yako mkubwa ameKatwa sikio, kwahiyo nashangaa hawa ndugu ambao wameongea kuhusu mimi kumkata sikio mama yangu mkubwa. Jamani mimi siwezi fanya kitu kama hicho. Kwanza sijaonanane muda mrefu sana.”
Rapper mkongwe, Godfrey Tumaini aka Dudu Baya ameingia kwenye orodha ya wahalifu wanaotafutwa na jeshi la polisi jijini Mwanza baada ya kumkata mama yake mkubwa sikio akidai ni mchawi.