Mwezeshaji Edda John Akielezea jambo kwenye Warsha iliyowahusisha Madiwani, Maafisa Watendaji wa kata na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kuhusu uelewa wa mpango wa Serikali wa TASAF [iii] iliyofanyika leo ktika ukumbi wa Ujenzi.
Madiwani, Watendaji wa kata na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Dodoma wakifuatilia jambo wakati walipokuwa kwenye Warsha ya kujengewa uelewa kuhusu mpango wa Serikali wa TASAF Awamu ya tatu.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Na John Banda, Dodoma
JUMLA ya kaya milioni 1.2 zinatarajiwa kufikiwa na mpango wa Serikali wa kupitia TASAF awamu ya tatu (TASAF III) kwa lengo la kunusuru kaya masikini katika wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Akizungumza kwenye warsha ya kutoa uelewa Madiwani,na watendaji wa Halmashauri hiyo ,Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TASAF ,Zuhura Mdungi alisema mradi huo unatekelezwa kwa kipindi cha miaka 10 katika awamu mbili za miaka mitano mitano.
Alisema,mpango huo umelenga kuzifikia kaya milioni 1.2 ambazo zinaishi katika hali masikini.
" Utekelezaji wa mpango huu unahitaji uwekezaji mkubwa kwenye mifumo na kujenga uwezo katika ngazi zote...,utatekelezwa kwa kuanza na maeneo machache na kuongeza maeneo zaidi kadri uwezo unavyojengeka na utekelezaji unavyoendelea." alisema Zuhura
Akielezea kuhusu madhumuni ya mpango,Zuhura alisema,ni kuwezesha kaya masikini sana kuongeza matumizi muhimu kwa njia endelevu,kuwezesha kuwa na matumizi wakati wa hari na kuwekeza kwenye rasilimali watu hususan kusomesha watoto.
Madhumuni mengine ni kuimarisha shughuli za kuongeza kipato na kuongeza matumizi ya huduma za jamii. Vile vile alisema,mpango wa kunusuru kaya masikini umeganyika katika maeneo mbalimbali ambayo ni kutoa ruzuku kwa kaya masikini sana hususan zenye wajawazito na watoto ili ziweze kupata huduma za elimu na Afya lakini pia kutoa ajira kwa kaya hizo masikini zenye watu wenye uwezo wa kufanya kazi wakati wa majanga mbalimbali.
Alisema ,eneo lingine la mpango huo ni kuongeza kipato kwa kaya masikini kupitia uwekaji akiba na shughuli za kiuchumi ili kuboresha maisha,kujenga na kuboresha miundombinu inayoenda sekta za elimu,Afya na maji lakini pia kujenga uwezo katika ngazi zote za utekelezaji.
Mpango huu Kitaifa ulizinduliwa Februari 2013 na Rais Jakaya Kikwete Mkoani Dodoma.