Kiukweli bado sijapata jibu la msingi kuhusu suala la kutupa taka kwenye hivi vifaa maalum vya kutunzia uchafu nabaki nikijiuliza maswali mengi hivi hakuna bajeti inayotengwa manispaa kwa ajili ya mafuta ya magari ya kubeba taka? Hivi hakuna magari maalum ya manispaa ya kubebea taka? maana magari yote yanayoonekana yakiwa yamebeba taka yana namba za private kwa hili bado sijapata jibu. Au ndo miradi ya watu? na bajeti yake inawekwa mifukoni mwa watu? Au majukumu ya usafi imepewa kata husika?
Kama kuna mtu yeyote mwenye jibu la msingi anifahamishe ili nijue.