Mtu mmoja amefariki dunia na 19 wamejeruhiwa na kuporwa vitu mbalimbali zikiwemo simu za mkononi na fedha baada ya majambazi kufunga barabara kwa mawe na magogo na kisha kuteka magari katika eneo la mkata doma barabara ya morogoro iringa.
Kwa mujibu wa kaimu kamanda polisi mkoa wa Morogoro John Laswai amesema tukio hilo limetokea majira ya usiku ambapo majambazi hao wakiwa na silaha mbalimbali waliteka magari na kujeruhi abiria ambapo aliefariki dunia amefahamika kwa jina la Richard Mgombea ambaye alifariki wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Morogoro na magari ya magazeti ya kampuni ya Mwananchi limetumbukia mtoni wakati wakijaribu kukimbia majambazi hao. Nao majeruhi waliolazwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro wakielezea tukio hilo wamesema wao ni madareva wa magari ya it na walikua wakitokea Mbeya kurudi Dar es salaam wakikutana na foleni kubwa barabarani ndipo wakatekwa na kujeruhiwa ambapo wamekiri kupoteza fedha mali na simu za mkononi.
Nae mganga wa zamu katika hospitali ya mkoa wa Morogoro Dr Erick Rwegoshora amekiri kuwepo kwa taarifa za kifo na wamepokea majeruhi wengine wamelazwa na wengine walitibiwa na kuruhusiwa .CHANZO ITV