Leo ni siku ya kumbukumbu ya kitaifa ya tangu kufariki kwa Sheikh Abeid Amani Karume miaka 42 iliyopita.Raisi huyo wa kwanza wa Zanzibar aliuawa kwa kupigwa risasi huko visiwani Zanzibar.
Ni uongozi wa Hayati Sheikh Amani Abeid Karume na Hayati Julius Kambarage Nyerere ambao ulitupa Tanzania tunayoijua hivi leo ukiwa ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar tangu mwaka 1964.
Kumbukumbu ya mwaka huu ya Sheikh Abeid Amani Karume inakuja huku bado kukiwa na “mpasuko” wa kisiasa huko visiwani hususani kuhusiana na suala zima la muafaka ambalo mpaka kufikia hivi sasa bado hayajapatikana maafikiano ya kueleweka.Ni imani yetu kwamba muafaka utakuja kufikiwa na amani itazidi kutawala.
Ili kujua au kujikumbusha vizuri historia ya Sheikh Abeid Amani Karume bonyeza hapa na hapa bila kusahau kutembelea mtandao wa zanzinet.org ambao umesheheni mambo mbalimbali kuhusu visiwa vya Zanzibar ikiwemo pia historia kamili ya visiwa hivyo. R.I.P Sheikh Abeid Amani Karume