Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

MKUU WA MKOA WA DODOMA DR. REHEMA NCHIMBI AFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA CHAMA CHA WALIMU (CWT) MKOA WA DODOMA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi akizungumza na wajumbe kwenye Mkutano wa Baraza la Chama cha Walimu Dodoma ambapo alisisitiza uwazi kwenye mapato na matumizi kutoka fedha za michango ya walimu ili kupunguza shutuma kwa viongozi wa CWT, Mkutano ulifanyika mapema leo kwenye ofisi za CWT Dodoma. 

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 
 Wajumbe wa Baraza la Chama cha Walimu (CWT) Mkoa wa Dodoma wakisikiliza salamu za Mkuu wa Mkoa Dodoma (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa baraza hilo ambapo viongozi hao wameaswa kuongeza uwazi kwenye mapato na matumizi ya michango ya walimu ili kujipunguzia shutuma kutoka kwa wanachama wao.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kulia) akiimba pamoja na wajumbe wa baraza la chama cha walimu Mkoa wa Dodoma wimbo unaowasisitiza walimu wote kuungana mapema leo kwenye Mkutano wa baraza la chama cha walimu Mkoa wa Dodoma.
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi, viongozi wa CWT Dodoma na wajumbe wa baraza la CWT Dodoma muda mfupi mara baada ya ufunguzi wa kikao cha baraza la CWT mkoa wa Dodoma mapema leo kwenye ofisi za CWT Mkoa.

Na John Banda, Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi amewataka viongozi wa chama cha walimu CWT kuongeza uwazi juu ya fedha za chama zinazotokana na michango ya walimu ili kupunguza shutuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha hizo kutoka kwa wanachama wa CWT/walimu.

Rai hiyo ilitolewa leo mjini Dodoma wakati wa Mkutano wa Baraza la CWT Mkoa wa Dodoma ambapo Mkuu huyo wa Mkoa amewataka viongozi waliopewa dhamana ndani ya CWT kuhakikisha wanaweka uwazi kwa wanachama wao wote juu ya namna michango ya walimu inavyokusanywa na jinsi inavyotumika

kwenye miradi ya maendeleo na shughuli nyingine za uendeshaji.

Aidha, Dr. Nchimbi ametaka pia viongozi hao kuwashirikisha zaidi wanachama kwenye kupanga mipango mikakati na kuibua miradi ya maendeleo na kusema kuwa kwa kufanya hivyo itawasaidia viongozi

kupunguza shutuma dhidi yao zinazotolewa na wanachama wa CWT kuwa baadhi ya viongozi wa CWT wamekuwa wakifanya ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha hizo zinazotokana na michango ya wanachama.

Vilevile Dr. Nchimbi amesisitiza CWT kuona umuhimu wa kuwaandaa walimu kustaafu hususani wale wanaokaribia kustaafu kwa kuwapa stadi za maisha baada ya kustaafu kwani maisha baada ya kustaafu kwa wengi ambao hawajajiandaa yanakuwa magumu mno.


Kwa upande wake Makamu wa Rais wa CWT Taifa ambae pia ni mkuu wa chuo cha ualimu bustani Kondoa Ndg. Honoratha Chitanda alibainisha kuwa ualimu ndio taaluma mama ya taaluma nyingine zote hivyo kuwataka waajiri na viongozi kutenga muda wa kukutana na walimu mara kwa mara kusikilizana changamoto na kutafuta ufumbuzi wa pamoja.


Nae Mwenyekiti wa CWT Dodoma Ndg. Augustino Njamasi amewataka wanachama wa CWT kutambua kuwa michango yao inafanya kazi ya kuwekeza miradi ya maendeleo akitolea mfano jengo jipya la CWT mkoa wa Dodoma.


Vilevile aliiomba serikali kupitia maafisa elimu Mikoa na Wilaya kushirikiana karibu na walimu kupitia CWT juu ya masuala mbalimbali ya utumishi wa walimu na kuongeza ombi kwa serikali kuongeza motisha za
 ufanyaji kazi bora kwa walimu ili kuwapa moyo wa kazi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>