Katika sherehe za kutimiza miaka kumi ya Mapinduzi 1974, Mwalimu Nyerere alikuwapo Zanzibar kufungua rasmi Televisheni Zanzibar TVZ ambapo kwa wakati huo ilikuwa ndiyo TV ya kwanza ya rangi Afrika Mashariki.
Pichani Ni Mkurugenzi wa TVZ Antony Mendis kulia kwa Mwalimu, Kamishna wa Polisi Zanzibar Edington Kissasi (Marehemu), Rais wa Zanzibar Aboud Jumbe Mwinyi nyuma ya Mwalimu, Waziri Kiongozi Ramadhaan Haji Faki aliyevaa baraghashia na Shaaban Mloo (Marehemu) nyuma ya Mendis.