Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

MATAJIRI/WATU WALIOFANIKIWA NA HADITHI YA USINGIZI WA ‘SAA NNE’, UNAHITAJI MASAA MANGAPI YA KULALA?

$
0
0
Kwa Gregory McKee, kupata usingizi mzuri usiku ni jambo muhimu kama kula chakula sahihi na kufanya mazoezi mara kwa mara. Asipopata usingizi wa saa nane, mwanzilishi na mkurugenzi huyo mtendaji wa kampuni ya La Jolla ya California, atakuwa na siku mbaya ya kufanya kazi siku inayofuata.
Miezi minne iliyopita, McKee alisafiri kwa ndege usiku kucha nje ya nchi kuhudhuria mkutano. Hakulala kabisa. Ilipofika katikati ya mchana, hali ilikuwa mbaya na alikuwa akitoka nje mara kwa mara kwenda kunywa kahawa na soda. Usiku wa siku hiyo, aligundua aliandika pumba tu kwenye karatasi za kuchukulia notice za mkutanoni.
Kwa upande mwingine, Darren Witmer hapati sababu ya kulala saa nane usiku. Huenda kulala sasa 9 usiku na huamka saa nne baadaye.

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mwenyekiti huyo mtendaji wa kampuni ya Cary, ya North Carolina inayojihusisha na kazi ya uelekezi wa biashara anadai huwa sawa kabisa siku inayofuata. Hasikii usingizi, hanywi kahawa sana na hapato shida kusoma notice zake mwisho wa siku.
“Ni ajabu kidogo,” alikiri. “Mke wangu ni mwanasaikolojia na amekuwa akiniangalia kwa mshangaO.”
Ni kiasi gani cha muda wa kulala; ni swali ambalo watu wengi huhangaika nalo. Licha ya tafiti mbalimbali zinazozungumzia umuhimu wa kupata usingizi wa kutosha, na kwamba tunahitaji kati ya saa saba au nane kila usiku – watu wengi hupata masaa machache ya kulala kwa sababu ya muda wa ziada kufanya kazi kuliko kuchukua muda huo kwaajili ya familia au matakwa binafsi.
Na ni ngumu kupuuzia ukweli wa wafanyabiashara waliofanikiwa kama Martha Stewart na Donald Trump, wanaodai kuwa hulala kwa saa tatu au nne tu kwa usiku. Maana yake ni kuwa: Mafanikio makubwa hayawezi kufikiwa hadi pale unapoutenga usingizi.
Hivyo, kulala kidogo ama zaidi kipi ni chema kwa career yako?
Watu wengi, popote wanapoishi duniani, huhitaji takriban masaa manane ya kulala ili kufanya kazi kwa ufanisi, anasema David Dinges, profesa wa saikolojia kwenye chuo kikuu cha Pennsylvania na mtafiti mahiri wa masuala ya usingizi nchini Marekani.

Madhara yaliyojificha
Eric Olson, mkurugenzi mwenza wa dawa ya usingizi kwenye kliniki ya Mayo ya Rochester, Minnesota, anasema umakini hupotea pale watu wanapolala chini ya masaa saba au nane kwa zaidi ya siku moja kwa kufuatana. Watu wanaolala kidogo hujikuta wakipata shida ya kuwa na kumbukumbu na hujikuta hatarini kuwa na matatizo ya kiafya kama kunenepa ama vifo vya mapema.
Kingine ni kuwa wale wanaolala kidogo na kutumia muda wa ziada kufanya kazi japo muda wanaotumia huwa si mzuri katika uzalishaji.
Witmer anakubali kuwa kufanya kazi kuanzia saa 3 usiku hadi saa nane si kwa kiwango kizuri katika kazi kama kufanya kazi kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni. “Huwa sifanyi vizuri saa nane usiku,” anasema. “Lakini uzalishaji wa asilimia 50 ni bora kuliko hakuna kabisa.”
Bado, wengi wanaolala kidogo wanaamini kuwa kiwango cha muda wanachotumia katika jambo fulani ni sababu ya kuendelea zaidi.
Hivyo, ni kweli kwamba kulala masaa matatu au manne kwa Donald Trump ndio chanzo cha mafanikio yake? Huenda si kweli, anasema Dinges. Watu kama Trumps hufanya kazi kwa ufanisi kwasababu hawana hofu ya mambo ya kila siku kama kulipa ada ama kutunza fedha kwaajili ya kustaafu. Matajiri huwa na timu ya watu wanaoshughulika na masuala ya kawaida kama kufua nguo, kulipa bili ama kupeleka watoto shule. Hali hiyo huwapa uhuru wakati wa masaa ya uzalishaji zaidi katika siku na kufocus zaidi kwenye kazi inayowafanya wafanikiwe.
Watu wanaolala kidogo huhofia uchovu kwa kulipiza masaa waliyopoteza ambapo wengi hulala zaidi wakati wa weekend kwa mfano. Mabosi walio busy hulala kwenye safari ndefu za ndege ama wakati wakipelekwa kwa gari katika mkutano. Mwanasheria Richard Bobholz ambaye naye hulala kwa masaa manne tu anasema mara nyingi hutumia dakika 45 kulala mchana.
“Nikiamka basi nakuwa tayari kuendelea tena,” anasema Bobholz.
Mwisho wa siku, kupata usingizi wa masaa manane ni muhimu, hasa katika mtazamo wa kuwa na afya njema, anasema Olson.
“Watu hawa wanaweza kuwa busy,” alisema Olson kuhusu wale wanaolala masaa manne, “lakini hawana ufanisi kama wanaotakiwa kuwa nao.”


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>