Itaendelea tena April 7 mwaka huu.
Pistorius anakabiliwa na kesi ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp Feb 14 mwaka jana
Kesi ya mauaji inayomkabili mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius imeahirishwa Ijumaa hii kutokana na mmoja wa wasaidizi wa kisheria wa Judge Thokozile Masipa anayeendesha kesi hiyo kuugua.
Timu ya Pistorius ilikuwa imejiandaa kuwasilisha utetezi wake Ijumaa hii huku yeye pia alikuwa akitazamiwa kusimama kizimbani. Kuahirishwa huko kunaipa timu yake wiki moja ya kujiandaa vyema na kesi hiyo.
Kama akipatikana na hatia, Pistorius, 27, anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka 25 jela.