Waziri mkuu wa Malaysia, Najib Razak akizungumza na vyombo vya habari baada ya kupata habari ya ndege ya Malaysia imeanguka kwenye bahari ya Hindi.
Shirika la ndege la Malaysia Airlines leo Jumanne limesema limetoa $5,000 ambazo ni takriban shilingi milioni nane kwa ndugu waliofiwa kufuatia ajali ya ndege yake ya MH370. Fedha hizi ni kwa kila abiria aliyekuwa kwenye ndege hiyo.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KBOFYA HAPA CHINI
Mwanamke mmoja alizidiwa na kubebwa na machela.
Limesema linajiandaa kutoa fedha zingine za ziada kuwasaidia ndugu hao. Jitihada za kutafuta mabaki ya ndege hiyo leo zimekwama kutokana na hali mbaya ya hewa katika bahari ya Hindi. Huko Beijing, mamia ya marafiki na ndugu wa abiria wa ndege hiyo waliandamana hadi kwenye ubalozi wa Malaysia kuelezea hasira zao.
Wanafunzi wa China wakiomboleza
Walidai kuwa walikuwa hawaambiwi ukweli wa kilichotokea kwenye ndege hiyo. Mamia ya polisi waliwazuia watu hao wasiingie kwenye jingo la ubalozi huo.
Hii ni mojawapo ya wasanii walivyoichora picha ya ndege ya Malaysia iliyoanguka kwenye bahari ya Hindi.
PICHA NA DAILY MAIL