Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) leo limetangaza rasmi matokeo ya mchakato wa kuwapata wateule rasmi wa vipengele 34 vya tuzo za muziki Tanzania. Akiongea na waandishi wa habari, Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey L. Mngereza amesema zaidi ya mapendekezo 30,000 yalitumwa kwa njia ya sms na mtandaoni.
Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA limeziondoa nyimbo tatu kwenye mchakato wa tuzo za muziki Tanzania, KTMA kwa madai kuwa zinakiuka maadili ya Kitanzania. Nyimbo hizo ni pamoja na ‘Nimevurugwa’ wa Snura, ‘Uzuri wako’ wa Jux na ‘Tema Mate’ wa Madee.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Madee akizungumza na Bongo5 leo baada ya kupata taarifa ya kuondolewa wimbo wake kwenye tuzo hizo, Madee amesema hajapendezwa na hatua hiyo.
“Sichukui hatua yoyote ila nawashangaa tu hao viongozi ambao wanahusika na mchakato mzima. Sisi tunaandika nyimbo ambazo vijana wetu wanazipenda,kwahiyo kama wameamua hivyo basi wawe wanatuandikia wao nyimbo,kwasasabu sisi tunawaandikia vijana wenzetu, sasa unakuta hao wanaoendesha mchakato ni wazee hawawezi kuchanganua maneno yetu,ifike time sasa wawe wanatuandikia mashairi,” amesema Madee.