Kituo kikuu cha mabasi yaendayo sehemu mbalimbali ndani ya mkoa wa Kilimanjaro na Arusha ikiwa haina gari baada ya wamiliki wa magari yaendyo maeneo hayo kugoma kutoa huduma. |
Ndipo askari walipoamua kuingilia kati na kuzuia mchezo huo uliokuwa hauna waamuzi wala milingoti ya kufunga magoli. |
Ulinzi ukaimarishwa zaidi. |
Baadhi ya makondakta na madereva wa magari hayo wakatiwa mikononi. |
Hata hivyo hatua ya kukamatwa kwa madereva na makundakta kiliwatia hasira wapiga debe wakaamua kulipopoa gari la polisi kwa mawe na kuvunja kioo cha nyuma kama inavyoonekana hapa. |
Abiria walilazimika kupanda gari la kusafirisha magazeti.Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii ,Moshi |