Lionel Messi akifunga katikati ya msitu wa wachezaji wa Real
Messi akiwanyooshea kidole mashabiki wa Barcelona baada ya kufunga, huku Gerard Pique (katikati) na Alexis Sanchez wakimfuata
Javier Mascherano na kipa Victor Valdes wakiwa chini, huku Benzema akitimka kushangilia baada ya kufunga.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Karim Benzema amefunga mabao mawili
Lionel Messi akiibusu nembo ya jezi ya Barcelona baada ya kufunga bao la ushindi katika El Clasico
Sergio Ramos akishangilia bao la tatu la Madrid na Ronaldo (kushoto) wakati nyota huyo wa Madrid anaonekana akiruka kulia Messi akafunga mara mbili mfululizo kwa penalti dakika za 65 na 84 kukamilisha hat trick yake Barcelona ikifufua matumaini ya kutetea ubingwa wake msimu huu.
Benzema akigombea mpira wa juu na Mascherano
Neymar akiwatazama Pepe na Fabregas wakifanyiana ubabe
Fabregas na Pepe wote waliishia kuanguka na wote wakaonyeshwa kadi za njano
Bale akipambana na Iniesta
Cristiano Ronaldo akilalamika baada ya kuchezewa rafu
Mashabiki wawili wa Real Madrid wakiwa na bango la kumtukuza Cristiano Ronaldo "Ameumbwa peponi".
MSHAMBULIAJI Lionel Messi amepiga hat-trick usiku huu Barcelona ikishinda 4-3 dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa La Liga uliofanyika Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid.
Andres Iniesta alianza kuifungia Barcelona dakika ya saba, Karim Benzema akaisawazishia Real dakika ya 20 na kufunga la pili dakika ya 24.
Barcelona ikazinduka na kupata bao la kusawazisha dakika ya 42 kupitia kwa Messi, lakini Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo akaifungia Real bao la tatu dakika ya 55 kwa penalti.
Real Ilimpoteza beki wake Sergio Ramos aliyetolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 63 kwa kumuangusha Neymar kwenye eneo la hatari, wakati Pepe, Di Maria, Alonso, Modric na Ronaldo wote walionyeshwa kadi za njano na kwa upande wa Barcelona, Fabregas na Busquets pia walionywa kwa kadi za njano. Kwa matokeo hayo Real inabaki na pointi zake 70, ingawa inaendelea kuongoza La Liga kwa wastani wa mabao, ikiwa inalingana pointi na Atletico Madrid, ambayo mapema iliifunga Real Betis 2-0, mabao ya Gabi dakika ya 58 na Diego Costa 64, wakati Barcelona inabaki nafasi ya tatu licha ya kufikisha pointi 69. Barca na Real zimecheza mechi 28 kila moja, wakati Atletico imecheza mechi moja zaidi. Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Diego Lopez, Pepe, Ramos, Cristiano Ronaldo, Benzema/Varane dk64, Bale, Marcelo, Xabi Alonso, Carvajal, Modric/Morata dk90 na Di Maria/Isco dk85. Barcelona: Valdes, Alves, Piqué, Mascherano, Jordi Alba, Sergio, Xavi, Iniesta, Fabregas/Sanchez, dk78, Messi na Neymar/Pedro dk69.
PICHA NA DAILY MAIL