Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

MFANYABIASHARA AUAWA KWA KUPIGWA JIWE KICHWANI HUKO TABORA

$
0
0
Hili ndilo jiwe alilopigwa nalo mfanyabiashara  wa vipuri vya pikipiki mjini Tabora marehemu Michael  Samson  na kupasua eneo kubwa la sehemu ya kichwa na kufariki papo hapo katika Bar ya Uhuru iliyopo mtaa wa Madrasat Kata ya Kanyenye manispaa ya Tabora.
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP SUZAN  KAGANDA akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu mauaji ya mtu mmoja ambaye alikuwa ni mfanyabiashara  wa vipuri vya pikipiki mjini Tabora marehemu Michael  Samson ambaye aliuawa usiku baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana ambapo walimpiga kwa jiwe kichwani lililosababisha kifo chake papo hapo.
 
Kwa mujibu wa mashuhuda mmoja kati ya wauaji mara baada ya kuwaamuru walale chini wateja watano waliokutwa kwenye Bar hiyo alichukua jiwe lililokuwa umbali wa hatua kumi na kuja kumpiga nalo mara mbili  kichwani  kwa nguvu marehemu Michael hali iliyosababisha kupasuka vibaya kichwa....Hata hivyo Polisi hadi sasa wanawashikilia watu wawili kuhusiana na tukio hilo la kinyama. 
CHANZO: KAPIPIJ BLOG

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>