Mazishi ya Sitti Mtemvu, mama wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu yaliyofanyika Dar es Salaam, Juni 2, 2017 katika makaburi ya Kinondoni ya kiongozwa na Mwenyekiti wa Bunge la Tanzania Mh, Azzan Zungu na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwepo Wananchi, Mkuu wa Majeshi Mstaafu Tanzania, Davis Mwamunyange , Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva, Wabunge wastaafu, Bi Sophia Simba, Mh, Adam Malima, Mh, Idd Azani, Mh, Vita Kawawa, na viongozi wengine akiwemo, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), MNEC wa Wilaya ya Temeke, Phares Magesa , Mbunge, Mariam Kisangi, Naibu Meya wa Kigamboni , Naibu Meya wa Temeke, Meneja wa DDC, Meneja wa Dawasco, Mh, Diwani wa Temeke, Kinondoni, Ilala, Mwenyekiti wa Vijana CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Omary Matulanga na Mkuu wa Idara ya Utawala UVCCM Taifa, Omary Mwanangwalu. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa ujijirahaa blog
Gari maalum lililoandaliwa na familia lakubeba mwili wa marehemu uliokuwa umehifadhiwa Hospitali ya Lugalo
Mtoto wa Marehemu Amina Mtemvu (katikati) akisaidiwa na mama mtemvu kushoto na kulia Hellen Mwilima baada ya kuutambua mwili wakati walipofika katika Hospitali ya Lugalo kuuchukuwa mwili wa marehemu kuelekea nyumbani kwa taratibu za mazishi
Mwili wa marehemu Sitti Mtemvu ukiingizwa katika gari maalumu ukitokea Hospitali ya Lugalo kuelekea nyumbani kwa taratibu za mazishi
Mwili wa Marehemu Sitti Mtemvu ukishushwa nyumbani
Wajukuu wa Marehemu Sitti Mtemvu wakiwa wamebeba picha ya marehemu
Mwili wa marehemu Sitti Mtemvu ukiwasili nyumbani ukipokelewa na waombolezaji ukitokea Hospitali ya Lugalo ukiingizwa ndani kabla ya kutowa heshima za mwisho
Mchungaji Huduma Neno lililopo Mbagala Mgeninani, Yohana Msumule akiongosa kwa Ibada fupi baada ya mwili kuwasili nyumbani
Familia ikiwa katika huzuni
Wadogo wa Mtemvu na Mh, Mtemvu wakiwa katika majonzi
Mdogo wa Marehem Hamisi Mtemvu akizungumza jambo na ndugu na familia yake baada ya yeye kutowa heshima za mwishi
Waombolezaji kwa kushirikiana na familia wakiuandaa mwili kwa kuuweka sehemu maalum ya kuagia
Sitti Mtemvu (kushoto) akizungumza na mama yake mama Mtemvu
Waombolezaji wakiwa wameubeba Mwili wa marehemu Sitti Mtemvu mara baada ya kukiwazili katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam
Mchungaji Huduma Neno lililopo Mbagala Mgeninani, Yohana Msumule akiongosa kwa Ibada fupi baada ya mwili kuwasili nyumbani
Waombolezaji
Mchungaji Huduma ya Maombezi Mbezi Beach Dar es Salaam, Atilio Komba, ambaye ni Mjukuu wa Marehemu Moris Nyunyusa (kulia) akitowa mahubilr katika makaburi ya Kinondoni kabla ya mazishi ya mama wa Mh, Abbas Mtemvu
Amina Mtemvu akitowa heshima za mwisho kwa kuweka udongo katika kabuli la mama yake
Aliyekuwa Mbunge wa Jibo la Temeke Mh, Abbas Mtemvu akitowa heshima za mwisho akiweka udongo katika kaburi la mama yake Juni 2, 2017 katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam
Mtoto wa marehemu Sitti Mtemvu, Herry Mtemvu akitowa heshima za mwisho akiweka udongo katika kaburi la mama yake Juni 2, 2017 katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam
Mh, Adam Malima akitowa heshima za mwisho kwa kuweka udongo
Mariam Mtemvu (kushoto) akitowa heshima za mwisho kwakuweka udongo
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), MNEC wa Wilaya ya Temeke, Phares Magesa akitowa heshima za misho
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Sharik Choughule (aliyevaa suti nyeusi) akiweka udongo katika kaburi la mama
Mkuu wa Majeshi Mstaafu Tanzania, Davis Mwamunyange, (kulia) akimpa pole aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu
Mh, Mtemvu na mkewe wakiweka shada la maua katika kaburi la mama yao
Mh, Malima akiweka shada la maua na mkewe katika kaburi la mama wa Mtemvu
Na Kamisi Mussa
Sitti Mtemvu ambaye alikuwa Mama wa aliyekuwa Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu amezikwa Juni 2, 2017 katika Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, ambapo Bi, Sitti Mtemvu alipata Elimuya yake ya msingi katika Shule ya Jamiatul Islamiya iliyopo Mtaa wa Lumumba na Aggrey wakati huo ukiitwa New street na Stanley street.
Marehemu, Sitti alifunga ndoa na Hayati Zuberi Mtemvu
mnamo miaka ya mwanzoni ya 1950, kipindi ambacho wote walijihusisha na shughuli za kisiasa za kudai Uhuru wa Tanganyika,
Wakati mumewe alikuwa Katibu wa kwanza wa Chama Cha TANU chini ya Hayati Mwalimu Nyerere, ambapo marehemu Sitti alijishughulisha na kuwahudumia wanasiasa hao wakati wapo kwenye mikutano ya siri iliyokuwa inafanyika nyumbani kwao
Kipindi hicho harakati za ukombozi zilikuwa zinafanywa kwa siri majumbani, ambapo nyumba ya
baba yake Marehemu Sitti iliyokuwa wanaishi ilitumika sana.
Harakati hizo ziliwashirikisha wakinamama, Maria
Nyerere, Sofia Kawawa, Bi Titi Mohamed na wengine, Marehemu pia alijiunga na vijana wengine kwenye mafunzo mbalimbali yaliyokuwa yanafanyika huko Arnatoglo Hall ambapo kulikuwa na mkusanyiko wa vijana wasomi waliojipanga kutawala Nchi yao.
Hapo ndipo chimbuko la Chama cha TAA na hatimaye TANU ilipoanzishwa , vilevile alijiunga na Elimu ya
watu wazima na kusoma Lugha ya Kiingereza. Mnamo miaka hiyo marehemu alisafiri mikoa
mbalimbali kuanza harakati za kudai uhuru dhidi mkoloni,
Marehemu aliwahi kuwa kiongozi wa ngazi
mbalimbali katika umoja wa wanawake wa Tanganyika wakati huo na hata na baada ya
Muungano wa Tanzania. marehemu alifanya kazi Tanzania Cigarette Company mnamo miaka ya 1965 na 1973 wakati huo BAT na Bank of Tanzania na kustaafu mwaka 1973.
Baada ya kustaafu marehemu alijishughulisha na biashara mbalimbali ikiwemo ufugaji wa kuku mnamo mwaka 1987 marehemu alihamia nchini Ivory Coast Abidjan na kufanya biashara ya kuendesha mgahawa
wa chakula kwa kushirikiana na familia yake.
Marehemu alilazimika kurudi nchni baada ya
machafuko ya kisiasa yaliyotokea nchini humo mnamo mwaka 1990.Marehemu alifariki mnamo Mei 30, 2017usiku kwa maradhi yaliyosababishwa na tatizo la sukarina umuri mkubwa
mwisho.