MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akifungua semina ya siku mbili ya fursa mpya ya kuongeza mapato ya halmashauri nchini kwa wakurugenzi wa majiji na manispaa iliyoandaliwa na shirika la maendeleo la UNCDF iliyofanyika jijini Arusha jana.
Mratibu wa mfuko wa mitaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) Peter Malika akizungumza
Mratibu wa mfuko wa mitaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) Peter Malika akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo na kusema,mpango huo wa kuwezesha halmashauri za majiji na manispaa, umeanza kwa majiji matato na manispaa tatu.
Baadhi ya wakuregenzi wa majiji na Manispaa waliohudhuria
SHIRIIKA la maendeleo ya mitaji la umoja wa Mataifa(UNCDF), jana limezindua mpango wa kuziwezesha halmashauri za majiji na Manispaa kuweza kunufaika na masoko ya mitaji kwa kuwekeza katika soko la la hisa kuuza vipande na kutoa hati za dhamana.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, alizindua mpango huo jijini hapa kwa niaba ya Waziri wa nchi ofisi za Rais(TAMISEMI) George Simbachawene na kuwataka watendaji na halmashauri za majiji na manispaa ,wanaohudhuria mafunzo hayo kujiandaa kutumia fursa hiyo.
Gambo alisema katika mpango huo, ambao unatarajiwa kuongeza mapato kwa halmashauri za majiji na manispaa nchini, kutokana na kuelimisha ni jinsi gani wataweza kuwekeza katika soko la hisa na kupata fedha za miradi ya maendeleo.
Alisema mpango huo, ambao unataribiwa na UNCDF unaziezesha halmashauri kupata fedha nyingi ambazo zitawezesha kuendesha miradi mikubwa ya miundombinu na hivyo kuchochea wanannchi.
Awali, Mratibu wa mfuko wa mitaji wa umoja wa mataifa(UNCDF) Peter Malika alisema,mpango huo wa kuwezesha halmashauri za majiji na manispaa, umeanza kwa majiji matato na manispaa tatu.
Malika alisema Majiji ambayo yatakuwa katika mpango huo ni Dar es Salaam,Mwanza, Arusha, Mbeya na Tanga na Manispaa ambazo zitahusika ni Kinondoni,Temeke,Ilemela na Dodoma.
"Majiji haya na manispaa wanauwezo wa kuanza kuwekeza katika masoko ya hisa kwa kuuza hati za dhamana na wataweza kupata fedha kwa miradi mikubwa ya maendeleo"alisema.
Mkurugenzi wa jiji la Arusha, Athuman Kihamia, alisema mpango huo tayari umeonesha mafanikio katika majiji kadhaa, ikiwepo Afrika Kusini, Marekani na Asia na wanatarajiwa utaboresha mapato ya halmashauri.
Kihamia alisema jiji la Arusha tayari limejiandaa kunufaika na mpango huo na tayari lina kampuni ya Arusha Investment ambayo inaweza kushiriki katika masoko ya hisa.