Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imetoa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Maofisa Mipango wa Halmashauri za Wilaya wa Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu kuhusu uandaaji wa mipango mikakati ambayo itatumika katika halmashauri za mikoa hiyo.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa, John Mongela alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa watumishi hao kwani yatawasaidia kupata mbinu mpya ambazo watazitumia wakati wa kutengeneza mipango mikakati katika maeneo yao.
Alisema kwa dhamana waliyonayo watumishi hao ni vyema kutumia mafunzo hayo ya siku mbili vizuri ili baada ya mafunzo waweze kupata njia mbadala katika uandaaji wa mipango mikakati ambayo itasaidia kuleta maendeleo
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa, John Mongela akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Maofisa Mipango wa Halmashauri za Wilaya wa Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu kuhusu uandaaji wa mipango mikakati
“Hampo hapa kwa ajali, mpo kwasababu dhamana zenu ni kubwa, kwa kupitia mafunzo haya mtapata nyezo za kupangia mikakati ya kweli na mimi nataraji mtatoka hapa vizuri, haya ni mafunzo muhimu sana, “Tusiishie kwenye mikakati, tatizo ni jinsi gani ya kuanzisha miradi, tumekuwa na mawazo mengi sana lakini tuna changamoto ya kuyaweka kwenye miradi, tutoke kwenye kuwa na mawazo na sasa tuanze kuyafanyia kazi,” alisema Mongela.
Pia Mongela aliwashukuru ESRF kwa kuandaa mafunzo hayo na kuwataka washiriki kufanya kazi kwa ushirikiano na ESRF kwani tayari wameonyesha nia ya kushirikiana nao ili kuhakikisha mipango ambayo wanaipanga inafanyiwa kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwenye mafunzo kwa watumishi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Maofisa Mipango wa Halmashauri za Wilaya wa Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu kuhusu uandaaji wa mipango mikakati.
“Tuone jinsi gani tunatumia fursa hii vizuri, tunatakiwa tukitoka hapa tukatekeleze mipango hii na ESRF wapo tayari kushikana mikono na sisi hadi waoane mafanikio na mimi niwahakikishie sisi tupo tayari … nategemea mambo makubwa baada ya kuanzisha ushirikiano huu,” alisema Mheshimiwa Mongela.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida alisema kwa kipindi kirefu wamekuwa mstali wa mbele kusukuma mbele Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa kufanya shughuli mbalimbali ambazo zinakuwa muhimu kwa maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla. “Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, wa nje na ndani ya nchi, ESRF imekuwa ikisimamia na kuhimiza ufikiwaji wa malengo hayo sio tu katika ngazi ya Taifa bali pia katika ngazi ya wilaya na hata Kata,” alisema Dk. KidaMkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa, John Mongela (katikati) akizindua mwongozo wa kuandaa mipango mkakati ya wilaya.
Dk. Kida aliendelea kusema kuwa mafunzo hayo kutakuwa na mada zinazoelezea maelezo ya Jumla kuhusu mpango mkakati, upangaji wa bajeti, ufuatiliaji na namna ya kutoa taarifa, mikakati ya maendeleo ya kitaifa na kimataifa SDGs, FYDP II, Africa Agenda 2063, Vision 2025, mchakato wa kuandaa mpango mkakati na ufuatiliaji, upimaji, na utoaji wa taarifa (reporting, monitoring and evaluation)
Aidha ESRF imezindua mwongozo wa kuandaa mipango mkakati ya wilaya, mwongozo ambao umetokana na andiko kubwa lililoandaliwa na serikali siku za nyuma kuhusu uandaaji wa mipango mkakati ya muda wa kati pamoja na bajeti (Government’s Medium Term Strategic Planning and Budgeting Manual).
Meza kuu ikionyesha mwongozo huo baada ya kuzinduliwa rasmi.Bwana Apolinary Tamayamali kutoka Ofisi ya Rais-IKULU akitoa neno kwa washiriki kuhusu mipango na mchakato wa uandaaji bajeti.Picha juu na chini ni Mkurugenzi Mtendaji wa Self Microfinance Fund, Mudith Cheyo akitoa mada kwa washiriki kuhusu uandaaji wa mipango mikakati.Picha juu na chini ni Washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa mipango mikakati ambayo yamehusisha watumishi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Maofisa Mipango wa Halmashauri za Wilaya wa Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu.Picha juu na chini ni Washiriki wa mafunzo kuhusu uandaaji wa mipango mikakati wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa, John Mongela.