Bustani ambayo imehifadhi historia ya vita kuu ya kwanza ya dunia (1914-1918)ikiwa na Sanamu ya askari Mwafrika katika sare ya kijeshi ya King's African Rifles aliyeshika bunduki yenye kisu cha kando na kutazama upande wa bahari, imefanyiwa ukarabati mkubwa na Kampuni ya kizalendo ya Green Waste Pro Ltd. Kampuni hiyo kama sehemu ya kurejesha faida kwa jamii ilitengeneza bustani hiyo iliyozinduliwa jana kwa gharama zake wakisimamiwa na mamlaka husika za wilaya na halmashauri. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bustani hiyo iliyofungwa kwa muda mrefu kwa ajili ya ukarabati kwenye msafara wa mbio za Mwenge, Meneja Msaidizi wa Green WastePro, Erick Mark alisema wamefurahi kwa mwenge kuzindua bustani hiyo inayorembesha mji na kuufanya uwe nadhifu
Muonekano wa bustani ya Askari monument kabla ya kuzinduliwa rasmi.
Sanamu hiyo iliyowekwa 1927 na Waingereza kama kumbukumbu ya askari na wapagazi Waafrika waliopigana vita Afrika ya Mashariki iliyomuondoa Mjerumani, iliondoa sanamu ya mtawala wa kijerumani Hermann VonWissman iliyowekwa mwaka 1911.
Eneo hilo ambalo sasa lina muonekano unaong'aa zaidi kutokana na kazi iliyofanywa na kampuni hiyo, ni sehemu ya kampeni kubwa ya kampuni ya Green WastePro Ltd iliyoanzishwa mwaka 2011 ikiwa na lengo la kusaidia halmshauri ya manispaa ya Ilala kuwa safi, ya kushawishi wakazi wa Dar kuupenda mji wao na kuusaidia kuuweka bora. Akifafanua zaidi kuhusu mradi wa upendezeshaji bustani ya sanamu ya askari maarufu kama Askari Monument, Mark alisema kazi waliyofanya ni kushawishi watanzania kutambua umuhimu wa usafi na kuringia kuwa na jiji safi hasa katikati ya Jiji. Kiongozi wa mbio za mwenge, Amour Hamad Amour akiwa ameshika mwenge baada ya kufika mtaa wa Posta Mpya jijini Dar kwenye uzinduzi wa bustani ya Askari Monument katika manispaa ya Ilala iliyokarabatiwa na kampuni ya Green WastePro ltd.
Alisema wanakazi kubwa ya kukabiliana na changamoto za ongezeko la takataka na udhibiti wa uchafuzi wa mazingira hususani hapa katikati ya jiji la Dar es salaam kwenye kitovu cha taifa, kazi ambayo wao wamekuwa wakifanya kwa ufanisi mkubwa usiku na mchana, bila kuchoka toka mwaka 2012 walipopewa dhamana hiyo na Halmashauri ya manispaa ya Ilala kwa mara ya kwanza.
Mbali na kazi hiyo pia wamekuwa wakijihusisha na shughuli mbalimbali za kijamii kwa utaratibu wa kujitolea (Corporate Social Responsibility) kama vile upandaji wa miti, utoaji wa vifaa vya kuhifadhia taka mashuleni, usafishaji wa fukwe, utoaji wa vifaa vya kuhifadhia taka na utunzaji wa mazingira maeneo mbalimbali ya jiji letu la Dar es Salaam hususani kwenye Halmashauri yetu ya Manispaa ya Ilala. Mkuu wa Idara ya usafi na mazingira Manispaa ya Ilala, Abdon Mapunda akisoma risala kwa mgeni rasmi ambaye ni kiongonzi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2017, Bw. Juma Khatibu Chum (hayupo pichani).
Akizungumzia mafanikio ya Kampuniya Green WastePro Ltd tangu ianzishwe, Mark alisema wameweza kutengeneza ajira zaidi ya 350 za kudumu pia wamefikia asilimia 80 ya uondoshwaji wa taka ngumu toka Julai 2012, ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo taka ziliondoshwa kwa asilimia 30% hadi 40. Pia wameweza kupanda miti maeneo mbalimbali kiasi cha miti 1,500 ndani na nje ya manispaa hii ya Ilala kwa miaka mitano iliyopita.
"Mafanikio mengine ni huu mradi tunaouzindua leo wa ukarabati mkubwa wa bustani hii yenye historia kubwa kwa jiji letu la Dar es salaam bustani ya picha ya askari ibismini maarufu kama (Askari monument) nadhani wote tunajionea palivyopendeza, mwenye macho haambiwi tazama." alisema. Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ndugu Amour Hamad Amour (kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kushoto) wakisikiliza hotuba ya Mkuu wa Idara ya usafi na mazingira Manispaa ya Ilala, Abdon Mapunda aliyokuwa anaiwasilisha kwenye uzinduzi wa bustani ya Askari Monument jijini Dar es Salaam kwenye mbio za Mwenge Kitaifa.
Hata hivyo alisema pamoja na mafanikio hayo, kampuni hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo tatizo la wizi. "Kwenye mradi huu wezi waliiba minyororo mara mbili. Pia kwenye mradi wa upandaji miti, nayo pia imekuwa ikiibiwa.Pindi tunapomaliza kuipanda hupita watu na kuifukua na kwenda kuiuza tena maeneo mengine. Changamoto ni nyingi sana ila hizi tumezitaja kwani zinahusiana na mradi huu." alisema Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (kushoto) akipiga makofi mara baada ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ndugu Amour Hamad Amour kuzindua mradi wa uboreshaji na utunzaji wa mazingira wa Bustani ya Askari Monument katikati ya jiji la Dar Es Salaam uliodhaminiwa na kampuni ya Green WastePro ltd.
Uongozi wa kampuni hiyo hata hivyo ulimwambia Kiongozi wa Mbio za Mwenge na msafara wake kwamba wana matarajio makubwa ya kuanza ukarabati wa bustani ya makutano ya barabara ya Barack Obama na Ali Hassan Mwinyi maarufu kama bustani ya (salender bridge) ili kuendelea kubadilisha mwonekano wa jiji la Dar es Salaam. Aidha kampuni hiyo inategemea kuanzisha mradi wa kuchakata taka ili kupunguza takataka zinazopelekwa dampo na pia kuzalisha ajira nyingine kwenye kazi hiyo na kuongeza kipato cha serikali upande wa kodi. Meneja Msaidizi wa kampuni Green WastePro ltd, Erick Mark akitoa ufafanuzi bustani ya Askari Monument iliyotengenezwa na kampuni hiyo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ndugu Amour Hamad Amour iliyozinduliwa Posta Mpya jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Green Waste Pro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo (kulia) akipokea mkono wa pongezi kutoka kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ndugu Amour Hamad Amour mara baada ya kumaliza uzinduzi wa mradi wa uboreshaji na utunzaji wa mazingira wa Bustani ya Askari Monument katikati ya jiji la Dar Es Salaam uliodhaminiwa na kampuni hiyo. Viongozi wa mbio za mwenge wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Ilala wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema mara baada ya kuzindua Bustani ya Askari Monument ambao ni mradi wa uboreshaji na utunzaji wa mazingira wa bustani hiyo katikati ya jiji la Dar Es Salaam uliodhaminiwa na kampuni ya Green WastePro Ltd. Wananchi waliojitokeza kwenye hafla ya uzinduzi wa bustani ya Askari Monument uliofanywa na Mwenge wa Uhuru katika eneo la Posta Mpya jijini Dar es Salaam. Wafanyakazi wa Green Waste Pro Ltd wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye bustani ya Askari monument jijini Dar es Salaam baada ya kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru.
Muonekano wa maua yaliyopandwa kuzunguka bustani ya sanamu ya bismini. Muonekano wa bustani ya Askari monument ikiwa imeshamiri maua ya kupendeza.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Green WastePro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo katika picha ya kumbukumbu kwenye bustani hiyo.
Muonekano wa usiku wa bustani ya Askari monument.