Mkuu wa Utawala na Uendeshaji wa Bohari Kuu ya dawa Zanzibar akitoa maeleza ya utendaji kazi wa aliekuwa mfanyakazi wake Abdalla Suleiman aliemaliza muda wa utumishi Serikalini katika sherehe zilizofanyika Ofisini kwao Maruhubi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Aliekuwa mkuu wa Kitengo cha kusambaza dawa Zanzibar Abdalla Suleiman akiwa na mke wake Dkt. Aza Said wakimsikiliza Mkuu wa Utawala na Uendeshaji Bohari Kuu ya dawA katika sherehe za kumuaga zilizofanyika Maruhubi.
Mkurugenzi Utumishi na Uendesha Wizara ya Afya Zanzibar Ramadhan Khamis Juma, aliekuekuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo, akimpongeza mstaafu Abdalla Suleiman kwa kukamilisha majukumu yake vizuri Serikalini.
Aliekuwa Mkuu wa Kitengo cha kusambaza dawa Zanzibar Abdalla Suleiman akiwapa mkono wa kwaheri wafanyakazi wenzake katika sherehe za kumuaga, wa kwanza (kushoto) Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya dawa Zahran Ali Hamad na (kati) Mkurugenzi Utumishi na Uendeshaji Wizara ya Afya Ramadhan Khamis Juma.
Mkurugenzi Utumishi na Uendeshaji Wizara ya Afya Ramadhan Khamis Juma akimkabidhi cheti cha utumishi bora aliekuwa Mkuu wa Kitengo cha kusambaza dawa Zanzibar Abdalla Suleiman ambae amestaafu kazi kwa mujibu wa sheria.
Picha ya pamoja ya mstaafu wa Bohari Kuu Abdalla Suleiman akiwa na mke wake Dkt. Aza Said (kulia) waliokaa na baadhi ya wafanyakazi wa Bohari kuu ya dawa na Ofisi ya Mfamasia Mkuu katika sherehe za kumuaga zilizofanyika Bohari Kuu ya dawa Maruhubi.
Picha na Makame Mshenga.