Nahodha wa Simba, Jonas Mkude anaendelea vizuri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ambako amefanyiwa vipimo na kupata matibabu kwa ujumla.
Mkude alikuwa kati ya watu sita waliopata ajali iliyotokea leo na shabiki mmoja wa Simba, Shose Fidelis amepoteza maisha.
Ajali hiyo ilitokea siku moja tu baada ya Mkude kuingoza Simba kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Kiungo huyo alifikishwa Muhimbili kwa matibabu zaidi ili kupata uhakika.
Lakini hali yake inaonekana kuimarika na imeelezwa jana alikuwa akilalama sana maumivu lakini sasa ana nafuu.
“Anaendelea vizuri, labda tuangalie kidogo kujua zaidi,” alisema mmoja wa viongozi wa Simba.