Mkufunzi wa Mafunzo, Wakili Dominic Ndunguru akielezea kuhusu ripoti ya utafiti ya shirikisho la dini (Interfaith standing committee) iliyozinduliwa Mwezi Mei mwaka 2017 kwa kuwashirikisha kamati ya kudumu ya Bunge ya Uchumi na Fedha inaliyoonyesha kuwa Tanzania kwa sasa inapoteza takribani dola bilioni 1.83 sawa na Tsh trilioni 4.09 kwa mwaka kupitia misamaha ya kodi, uhamishaji wa fedha nje ya nchi bila kufuata utaratibu, kushindwa kutoza kodi sekta isiyo rasmi na aina nyingine za ukwepaji kodi.
Meneja Mradi Wa Elimu ActionAid Tanzania, Karoli Kadeghe akiwasilisha mada kuhusu mtazamo wa upatikanaji wa elimu nchini Tanzania wakati wa Mafunzo ya wanachama na viongozi wa Chama cha Walimu na Asasi za Kiraia waliokutana mkoani Singida yaliyofanyika kwa siku tatu.
Mdau wa Elimu kutoka asasi za kiraia, Lucy Mkosamali akichangia mada ya umuhimu wa uwekezaji katika maendeleo ya sekta ya elimu kwenye mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida ulioandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
Mwenyekiti wa Chama wa walimu Wilaya ya Singida, Bw. Hamisi Mtundua akichangia mada kwa kutoa uzoefu wake kuhusu maslahi ya walimu na miundombinu ya shule za vijijini kwenye mafunzo yaliyofanyika mkoani humo.
Afisa Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Bi. Alistidia Kamugisha akichangia mada kwenye mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida ulioandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
Washiriki wa mafunzo wakifanya kazi za makundi kuhusu haki ya kupata elimu bora kwenye mafunzo yalioandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
Mwakilishi wa Walimu Wanawake Chama cha walimu Manispaa ya Singida, Bi. Innosanta Shayo akiwasilisha kazi ya kikundi cha Tano waliyokuwa wakijadili jinsi ya mtoto kupata haki katika elimu.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa elimu mkoani Singida wakifuatilia mafunzo
Mratibu wa Elimu kata ya Mtinko akichangia mada ya haki za watoto mashuleni pamoja na Umuhimu wa ukusanyaji wa mapato ya ndani kuwekeza katika sekta ya elimu kwenye mafunzo yaliyoandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
Meneja Mradi Wa Elimu ActionAid Tanzania, Karoli Kadeghe akiwaelekeza washiriki wa mafunzo namna ya kuhamasisha haki za watoto mashuleni kwa vitendo kwenye mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida yalioandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
Afisa Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Bi. Alistidia Kamugisha akitoa uzoefu wake kuhusu kuhamasisha haki za watoto mashuleni wakati wa elimu ya vitendo kwenye mafunzo ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto za utoaji wa elimu bora hapa nchini mkutano huu uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida yalioandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
Washiriki wa mafuzo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mafunzo yaliyofanyika kwa takribani siku tatu mkoani Singida
Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) kwa kushirikiana na ActionAid Tanzania waliandaa mafunzo ya siku tatu kwa wanachama wa chama cha walimu na asasi za kiraia za elimu mkoa wa Singida kuhamasisha upatikanaji wa haki za mtoto shuleni na maendeleo ya sekta ya elimu kwa kushawishi serikali kuongeza uwekezaji katika sekta ya elimu kwa kutumia rasilimali za ndani.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Meneja Mradi kutoka ActionAid Tanzania Karoli Kadeghe alielezea katika bajeti ya elimu 2016/17, takribani bilioni 277 sawa na asilimia 31% ilitarajiwa kukusanywa kutoka kwa wahisani na washirika wa maendeleo. Hata hivyo, hadi kufikia mwezi Machi 2017, wahisani walikuwa wametoa kiasi cha shilingi bilioni 132 tu sawa na asilimia 47.6%. Alisisitiza kuwa ni vyema serikali iimarishe vyanzo vyake vya mapato vya ndani ili kuepuka aibu hii na sisi wadau wa elimu tunalo jukumu la kuisimamia serikali katika kutimiza wajibu wake. Kila mtu akilipa kodi stahiki kadiri ya kile anachozalisha na pia serikali ikidhibiti mianya ya upotevu wa kodi, hata kodi ya PAYE itapungua na kumpa mwalimu ahueni katika makato hayo.
Mkufunzi wa Mafunzo hayo Wakili Dominic Nduguru akiwasilisha mada juu ya ulipaji wa kodi na Uwekezaji katika Elimu alitumia ripoti ya utafiti ya shirikisho la dini (Interfaith standing committee) iliyozinduliwa Mwezi Mei, 2017 kwa kuwashirikisha kamati ya kudumu ya Bunge ya Uchumi na Fedha inaonyesha kuwa Tanzania kwa sasa inapoteza takribani dola bilioni 1.83 sawa na Tsh trilioni 4.09 kwa mwaka kupitia misamaha ya kodi, uhamishaji wa fedha nje ya nchi bila kufuata utaratibu, kushindwa kutoza kodi sekta isiyo rasmi na aina nyingine za ukwepaji kodi. Pia alidokeza ripoti kadhaa zinazoonesha upotevu au ukwepaji wa kodi unaofanywa na makampuni ya kigeni na wawekezaji wakubwa ambao unaathiri uwekezaji katika uboreshaji wa huduma za jamii hususani sekta ya elimu.
Washiriki wa mafunzo hayo kutoka chama cha walimu na asasi za kiraia za elimu mkoa wa Singida wamejengewa uwezo katika maeneo mbalimbali ikiwemo Nguvu ya kodi, haki za binadamu, haki ya watoto mashuleni, ushawishi na utetezi wa maslahi ya walimu na haki za watoto, umuhimu wa ukusanyaji wa kodi na rasilimali za ndani ili kuboresha miundombinu ya elimu na ubora wa elimu.
Viongozi na wanachama wa chama cha walimu pamoja na asasi za kiraia za elimu mkoani Singida wameazimia kuyafanyia kazi mafunzo hayo na kuungana kwa pamoja kwa kutengeza Mtandano wa Elimu Singida ili kushawishi mamlaka na serikali kusimamia ukusanywaji wa mapato ya ndani ili kuboresha sekta ya elimu. Washiriki walichagua uongozi wa mpito wa Mtandao wa Elimu Singida na kuchagua taasisi ya Youth Movement for Change kama sekretarieti ya muda.