Rais wa John Magufuli ameeleza sababu kwa nini alimfukuza kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa.
Rais Magufuli amesema kuwa alichukua uamuzi huo kutokana na Profesa huyo kueleza Kamati ya Bunge kiasi ambacho kilikuwa kipo kwenye makontena ya dhahabu ambacho hakikuwa sawa.
Profesa Ntalikwa alifutwa kazi na Rais Magufuli siku chache baada ya kufanya ziara ya kushtukiza bandarini lakini hakubainsha iwapo kuna uhusiano kati ya ziara hiyo na kufutwa kwake Ntalikwa.