Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (Mbele) akihutubia maelfu ya wanafunzi wa shule za sekondari za jijini Arusha zinazoshiriki michuano ya Copa/UMISSETA, katika ufunguzi wa mashindano hiyo mkoani Arusha kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid iliyofanyika mwishoni mwa wiki. Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (Mbele) akiambatana na Meneja wa Mauzo wa Coca-Cola kwa Jiji la Arusha Boniface Mwasi, wakisalimia wachezaji wa moja ya timu za sekondari zinazoshiriki michuano ya Copa/UMISSETA, katika ufunguzi wa mashindano hiyo mkoani Arusha kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (Kushoto) akisalimia moja ya timu ya shule za sekondari kutoka mkoa wa Arusha, katika ufunguzi wa mashindano ya Copa Umisseta mkoani hapa yaliyofanyika mwisho wa wiki katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, ambapo kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola iligawa vifaa mbali mbali vya michezo kwa shule za serikali na binafsi kwa ajili ya ushiriki wa michuano yam waka huu.
Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola hapa nchini, kwa ushirikiano na TAMISEMI, imefanya uzinduzi wa mashindano ya umoja wa shule za sekondari (Umisseta) kwa kanda ya Kaskazini, mkoani Arusha kwa kugawa vifaa vya michezo kwa shule mbalimbali za sekondari za serikali na binafsi. Katika uzinduzi wa mashindano hayo jijini Arusha, kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid mwishoni mwa wiki, mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha - Mrisho Gambo, ambapo aliishukuru kampuni ya Coca cola kwa udhamini kufanikisha michuano yam waka huu. Kwa upande wake, Meneja Mauzo wa Coca-Cola mkoa wa Arusha, Boniface Mwasi alisema kuwa kampuni hiyo imeona umuhimu wa kuibua vipaji vya michezo ndio maana wamejikita kufadhili michezo kama hiyo kwa vijana.
“Tumeamua kushirikiana na serikali katika michezo hii ya Umisseta lengo letu kubwa likiwa ni kuibua vipaji vingi vya michezo kwa kuwa tunaamini mtandao wa shule za sekondari ni mkubwa na ni rahisi kuibua vipaji vingi kutoka sehemu zote za nchi”, Alisema Mwasi. Aidha, aliongeza ya kwamba kampuni ya Coca-Cola itaendelea kuunga mkono jitihaa za serikali za kukuza sekta ya michezo nchini hususani katika ngazi za chini ambako imekuwa ni vigumu kupata ufadhili kwa kuwa tunaamini kuwa vipaji vinapaswa kuibuliwa na kukuzwa. “Tunayo dhamira kuona vijana wa kitanzania walioibukia kwenye mashindano haya wanafika mbali kimichezo”, Alisisitiza Mwasi.