Watu 19 wameuwawa na wengine zaidi ya 50 wamejeruhiwa katika tukio linashukiwa kuwa ni shambulizi la kigaidi katika ukumbi wa Manchester Arena.
Mlipuko huo umetokea usiku wa jana wakati wa tamasha la muziki la mwanamuziki wa pop kutoka Marekani Ariana Grande.
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ametoa pole kwa wafiwa na waliojeruhiwa na tukio hilo ambalo polisi wanalichukulia kama shambulizi la kigaidi.
Mwanaume aliyejeruhiwa katika shambulizi la Manchester Arena
Watu waliokuwa kwenye tamasha wakijifunika na mifuko ya foili kujizuia na baridi