Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

JE WATAKA KUJUA: MAMBA ANANG'ATA KWA NGUVU KULIKO MNYAMA YEYOTE

$
0
0
MAMBA ni mnyama mwenye uwezo mkubwa wa kung’ata kwa nguvu zaidi kuliko mnyama mwingine yeyote. Kwa mfano, mamba wa maji ya chumvi wanaopatikana Australia, wanaweza kung’ata kwa nguvu mara tatu zaidi ya simba. Pia, taya la mamba lina uwezo wa hali ya juu wa kuhisi (sense). Uwezo huo unazidi ule wa ncha ya kidole cha mwanadamu.

Taya la mamba limefunikwa kwa maelfu ya mishipa ya hisia. Kila neva imeunganishwa na fuvu la kichwa,Mpangilio huo unalinda nyuzi za neva zilizo katika taya na kufanya sehemu fulani za taya ziwe na uwezo mkubwa wa kuhisi. Kwa sababu ya kuwa na uwezo huo, mamba anaweza kutofautisha mdomoni mwake kati ya chakula na uchafu. Hilo pia linamwezesha mamba jike kubeba watoto wake kwa kutumia mdomo bila kuwaua.

Imeandaliwa na Moses Mutente

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>