Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhe.Mwigulu Nchemba amewaonya wananchi wa Kibiti mkoa wa Pwani kutowaficha wahalifu wanaofanya mauaji mkoani humo bali wawafichue ila maisha yaweze kuendelea kama zamani na kudai pasipo kufanya hivyo kuna gharama.
Mhe. Mwigulu amewataka wananchi kutambua kwamba kuendelea kuwaficha wahalifu waliopo ndani ya jamii watambue kuna gharama kubwa ambayo itawafanya maisha yasiweze kusonga mbele.
Mwigulu ameyasema hayo jana Kata ya Bungu wilaya ya Kibiti mkoa wa Pwani mara baada yakutembelea majeruhi na kambi maalum ya jeshi la Polisi mkoani humo kwa ajili ya kupambana na waalifu ambao wanajihusisha na kuua wananchi ,viongozi wa dini na vyama.
Wakati akizungumza na wananchi pamoja na kikosi maalumu kilichopo huko, Mhe. Mwigulu amesema kwamba serikali imejipanga vyema kubana mianya ya wote wanaofanya mauaji hayo na kuongeza kwamba itawatia nguvuni, na kuwataka wananchi kuwa mstari wa mbele kuwafichua wahalifu hao
Nchemba ameendelea kufunguka kwamba uhalifu unaoendelea kwa sasa maeneo hayo ya Kibiti yanasababisha wasiwasi kwa wananchi na kuongeza kuwa serikali haitawaacha wahalifu waendelee kufanya mauaji hayo na kuongeza kwamba hakuna ruhusa ya aina yeyote ya mtu kumuua mwenzake kwa misingi yakua na mtazamo tofauti wa dini, chama , kabila na asili.
Pamoja na hayo ameongeza kwamba serikali imeanza kuwabaini wahusika wa vitendo hivyo na bado wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wahalifu wengine.
==>Msikilize hapo chini akiongea