Mabalozi wa Kundi la Mtandao wa Kijamii wa Whatsaap la Saratani Info wakiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC tayari kutembelea kitengo cha Saratani katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC.
Mabalozi wa Kundi la Mtandao wa Kijamii wa Whatsaap la Saratani Info wakiwa wamebeba zawadi mbalimbali kwa ajili ya kutoa kwa wagonjwa wa Saratani katika Hosptali ya Rufaa ya KCMC.
Mkuu wa Kitengo cha Saratani katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC,Dkt Furaha Silventi akizungumza na mabalozi wa kundi la Saratani Info lilipotmbelea kitengo hicho.
Mkuu wa Kitengo cha Saratani katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC,Dkt Furaha Silventi akizungumza na mabalozi wa kundi la Saratani Info lilipotmbelea kitengo hicho,kulia kwake ni Kiongozi wa Mabalozi hao kanda ya Kaskazini,Veri Njau na kushot ni Mratibu katika kitengo hicho Everlyn Ndosi.
Kiongozi wa Kundi la Mabalozi wa Saratani la Saratani Info kanda ya Kaskazini,Veri Njau akizungumza na baadhi ya wagonjwa pamoja na mabalozi hao baada ya kuwatembelea katika kituo cha Saratani ,KCMC.
Baadhi ya wagonjwa wa Saratani wanaopatiwa matibabu katika kitengo cha Saratani ,Hospitali ya Rufaa ya KCMC ambao kundi la Mabalozi wa ugonjwaa huo liliwatembelea na kutoa msaada wa gharama za Bima ya Afya kwa watoto nane (8).
Mabalozi wa Ugonjwa wa Saratani wakitembelea katika maeneo mbalimbali ya kitengo cha Saratani katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC.
Mmoja wa Mabalozi wa Ugonjwa wa Saratani wa kundi la mtandao wa WhatsApp la Saratani Info ,Respicius Baitwa akizungumza kabla ya kukabidhi fedha kwa ajili ya Bima za Afya kwa wagonjwa wa Saratani nane wanaopata matibabu katika kituo hicho.
Mkuu wa Kitengo cha Saratani katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC,Dkt Furaha Silventi akitoa neno la shukurani baada ya Mabalozi wa Kundi la WhatsApp la Saratani Info kukabidhi msaada wa fedha kwa ajili ya Bima za Afya kwa watoto nane wanaopata matibabu katika kitengo hicho.
Baadhi ya Mabalozi wa Saratani waliotembelea kitengo cha Saratani katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kuwaona wagonjwa wa Saratani wanaopata matibabu katika Hospitai hiyo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.