Teddy na Talkia Tumbi ambao ni mtu na dada yake wamefanya uzinduzi wa studio ya nywele na kuuza shanga na vito (jewelry) iliyopo kwenye mji wa Clemmons, North Carolina nchini Marekani. Studio hiyo ambayo ilizinduliwa siku ya Jumamosi May 13, 2017 ilihudhuriwa na Watanzania mbalimbali waliofika kuwaunga mkono.
Teddy Tumbi akimwandalia mteja (hayupo pichani)shanga alizonunua kwenye studio yao iliyofunguliwa siku ya Jumamosi May 13, 2017 Clemmons, North Carolina nchini Marekani. Studio hii ya kutengeneza nywele na kuuza shanga na vito (Jewelry) na anuani kamili ni 2575 Old Glory Road, Clemmons, NC 27012 simu 336 343 8170.
Talkia Tumbi mmoja ya wamiliki wa studio hiyo siku ya uzinduzi wake uliofanyika siku ya Jumamosi May 13, 2017 Clemmons, North Carolina nchini Marekani.
Mmoja ya wateja akitengeneza nywele zake.
Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi. Glory Alex akipata matunda ya ufunguzi wa studio hiyo kwa kutengeneza nywele zake alipokwenda kuwaunga mkono Teddy na Talkia Tumbi mtu na dada yake walipofungua studio ya nywele na kuuza shanga na vito.
Mmoja ya wateja akitengeneza urembo wa nywele studioni hapo.
Ulimbwende wa kucha ukiendelea
wasusi wakipata picha kwenye studio ya nywele na kuuza shanga na vito iliyofunguliwa siku ya Jumamosi May 13, 2017 Clemmons, North Carolina nchini Marekani.
Muonekano wa studio
Mwenyekiti Glory Alex akiwa katika picha ya pamoja na Teddy Tumbi mmoja ya wamiliki wa studio hiyo siku ya uzinduzi wake uliofanyika siku ya Jumamosi May 13, 2017 Clemmons, North Carolina nchini Marekani.
Mwenyekiti Glory Alex akiwa katika picha ya pamoja na Talkia Tumbi mmoja ya wamiliki wa studio hiyo siku ya uzinduzi wake uliofanyika siku ya Jumamosi May 13, 2017 Clemmons, North Carolina nchini Marekani.